Pages

Wednesday, May 22, 2013

KIUNGO KINDA WA TAIFA STARS MUDATHIR YAHYA AWAFUNIKA AKINA WAKONGWE STARS




Mudathir akiwa na mpira wakati wa mazoezi ya stars 



KIUNGO kinda mshambuliaji wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Mudathir Yahya jana alionekana kuwafunika washambuliaji Mrisho Ngasa na Salum Abubakar kwenye mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika Uwanja wa Karume.
Mudathir Yahya anayetokea Azam FC alionekana kumfurahisha kocha Kim Poulsen kutokana na uwezo wake wa kufuatilia mafundisho yake kwa vitendo walipokuwa kwenye mazoezi ya timu hiyo.
Mudathir ambaye ni mara yake ya kwanza kuitwa kwenye kikosi cha wakubwa, awali alikuwa kwenye timu ya vijana waliochini ya miaka 17 ‘Serengeti boys’, kocha alimwita kwenye stars ndogo na kuweza lkufanya vizuri na sasa yupo kwenye timu ya wakubwa ambako pia ameonyesha kuwa anaweza.
Kijana huyu ambaye ni mpole na siyo muongeji kutokana na jinsi alivyokuwa anacheza alijikuta akishangiliwa na mashabiki waliokuwepo uwanjani kushuhudia mazoezi hayo.
Alisikika shabiki akisema ‘Serengeti boys huyu atawanyang’anya namba mafadha sasa hivi maana yupo fiti na kocha anamkubali pia’.
Taifa stars ipo kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Morocco lakini pia kabla ya kurudiana na Morocco utakaochezwa Juni 8, mwaka huu lakini  itacheza mchezo wa kirafiki na Sudan, wakati wakiwa safari kwenda Morocco mchezo utakaochezwa nchini Ethiopia Juni 2, mwaka huu
Meneja wa Timu hiyo Taso Mukebezi alisema wachezaji wote wapo kambini na wana afya njema isipokuwa Mwinyi Kazimoto ana jereha dogo kwenye mguu ambalo lilitokana na kuchubuka wakati wa mazoezi ya asubuhi.
“Timu imekamilika isipokuwa Mwinyi Kazimoto amepumzika kwani asubuhi alipata mchubuko kwenye mguu na wachezaji Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata wataungana na timu Morocco wakitokea Congo”, alisema Mukebezi
Pia timu inaendelea na mazoezi kwenye  Uwanja wa Karume leo asubuhi na jioni hadi Mei 26, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment