Pages

Wednesday, May 22, 2013

PEREZ AFANYA KUFURU KUMSAJILI BALE



Klabu ya soka ya Real Madrid bado ipo katika vita kali ya ya kutaka kumsainisha winga machachari wa timu ya soka ya taifa ya Wales anayechezea Totenham Hot Spurs ambaye hivi karibuni ameaidiwa mshahara wa pauni laki moja na nusu   kwa juma  £150,000 sawa na shilingi miliano mi tatu sabini na tano unusu za Tanzania .

Mkataba huo utamfanya kuuzwa kwa pauni milioni hamsini kama atahitaji na timu nyingine msimu ujao (£50m). Lakini hilo halidhuru kitu kwa Rais wa klabu ya Real Mdrid Florentino Perez, ambaye anamtaka Bale kwa sasa.

Anasema atampatia pesa zaidi ya hiyo iliajiunge na The Galacticos. Kuna kandarasi ya miaka mitano mezani ambayo tutampatia Bale, mshahara zaidi ule anaupata hapo White Hart Lane.

Lakini hii itahusisha na haki za picha za mchezaji huyo ambao utamapatia fedha zaidi .
Japokuwa, Real inasisitiza kuwa hawawezi kulipa zaidi pauni milioni  £43m, ambacho ni kiwango cha chini zaidi na kile kilichowekwa na  Tottenham’s kwa mwaka .

Madrid imetoa ofa ya wachezaji wanne ikiwa kama fidia ya kumnasa mchezaji huyo wa Spurs wachezaji hao ni – Pepe, Marcello, Gonzalo Higuain na  Angel di Maria.
lakini mchezaji pekee ambaye pengine anaweza kuwa chambo kwa ajiri ya Spurs ni mshambuliaji Higuain lakini yeye mwenyewe ameshasema kuwa hataki kuondoka Santiago  Bernabeu na kwenda kuchezea klabu ambayo haichezi ligi ya mabingwa barani Ulaya jambo ambalo halijazima Ndoto za Real kwa sasa , Lakini real inasema Spur itamwachia mchezaji huyo kwa kwakuwa hata mwaka jana mwenyekiti wao  Daniel Levy alikuwa akisisitiza kuwa hawezi kumuuza   Luka Modric kwa real lakini baadae alimuuza kwao.

No comments:

Post a Comment