Pages

Thursday, May 16, 2013

MASHINDANO YA KUOGELEA YA TAIFA YANAANZA LEO KENYA


MASHINDANO ya kuogelea ya Taifa ya umri mdogo yamepangwa kuanza leo nchini Kenya, huku Tanzania ikipeleka waogeleaji 25.
Mashindano hayo ya siku tatu yamepangwa kufanyika katika bwawa la shule ya Aga Khan nchini humo na kushirikisha waongeleaji 2000 kutoka ukanda huu wa Afrika.
Katibu msaidizi wa Chama cha Kuogelea nchini TSA, Ramadhan Namkovela amesema kuwa mashindano hayo yanashirikisha vijana wenye umri wa miaka 11 kushuka chini.
Alisema kuwa Tanzania imepeleka waogeleaji wenye umri wa miaka 7 hadi 11, ambapo michuano hiyo itasaidia kukuza viwango vya waogeleaji hao.
Aliwataja waogeleaji hao kuwa ni Reuben Monyo, Njukia Kihara, Prashraad Magesvaran, Oliver McIntosh, Shiv Shreekumar, Gian Maria, Vansh Ladwa, Dhashraad Magesvaran, Alexander Belikov, Harry McIntosh, Urav Shah, Maia Tumiotto, Diya Patel, Amani Doggart.
Wengine ni Celina Itatiro, Tessa Francis, Janice Njuguna, Smriti Gokarn, Selina Mehta, Sonia Tumiotto, Maya Kihara, Mariana Pipollo, Piya Shah, Talin Stengel and Ursula Khimji.
Mkuu wa Msafara Inviolata Rwelamira-Itatiro, Kocha Mohamed Abdulaziz, Kocha Alex Mwaipasi, Kocha Kanis Mabena.

No comments:

Post a Comment