Pages

Thursday, May 16, 2013

MASHINDANO YA POOL TABLE VYUO VIKUU VYA DAR KUANZA KESHO


Oscar Shelukindo, ambaye ni meneja wa bia ya safari akizungumza na waandishi wa habari jana

Mwenyekiti wa chama cha Pool Table Taifa akiongea na waandishina washiriki 

Raymond Yamo wa DUCE akipokea vifaa kwa ajili ya timu yake toka kwa Oscar Shelukindo, Meneja wa bia ya safari Lager


Wshiriki wakipewa semina


 MASHINDANO ya mchezo wa pool kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam, yanayojulikana kama 'Safari Lager Higher Learning Pool Competition 2013' yanatarajiwa kufanyika Jumamosi na Jumapili kwenye Baa ya Meeda, iliyopo Sinza.
Akizungumza na waandishi wa habari jana wakati wa kukabidhi sare za kuchezea mchezo huo, Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo, alisema hiyo itakuwa ni hatua ya mwisho kwa upande wa mikoa kabla ya kuendelea katika mashindano ya Taifa ya mchezo huo, yatakayofanyika Juni Mosi jijini Dar es Salaam.
“Kama mtakumbuka kwamba tayari tumefanya mashindano ya ngazi ya mikoa na mabingwa wake wamepatikana, hii ni zamu ya Dar es Salaam,” alisema Shelukindo.
Katibu wa Chama cha Pool Taifa (TAPA), Amos Kafwinga, aliwashukuru wadhamini wa mashindano hayo Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Safari Lager kwa kuendelea kudhamini mashindano hayo.
“Tunawashukuru wadhamini wetu kwa mchango mkubwa katika mashindano haya, tumejipanga vizuri kuufanya mchezo huu uwe namba moja.
“Mashindano haya ya vyuo vikuu kwa Mkoa wa Dar es Salaam, yatafanyika kwenye Ukumbi wa Meeda na kushirikisha vyuo 15,” alisema.
Alivitaja baadhi ya vyuo hivyo kuwa ni DSJ, Mwalimu Nyerere, UDSM, Chuo Kikuu Huria (OUT), Kairuki, IFM, CBE, Ardhi, DUCE, DIT na IMCO.

No comments:

Post a Comment