Pages

Thursday, May 16, 2013

MABONDIA 10 KATI YA 16 WARIPOTI MAZOEZINI


IDADI ya mabondia wa timu ya taifa walioripoti mazoezini, imeongezeka na kufikia 10 badala ya 16 walioitwa kuunda kikosi hicho.
Timu hiyo ilianza mazoezi katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam Jumanne ya wiki iliyopita, ambapo mabondia wanne pekee ndio walikuwa wameripoti mazoezini kwa wiki hiyo.

Lenzi ya Michezo jana  ilishuhudia mabondia 10 wakifanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya kimataifa, ikiwemo ile ya Afrika wakati idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka zaidi ifikapo wikiendi hii.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Lemmy Ngabo amesema kuwa mabondia wengi ambao ni waajiriwa wa Taasisi mbalimbali zikiwemo Vyombo vya Ulinzi na Usalama, wameshapewa kibali cha kujiunga na timu hivyo kufikia Jumatatu huenda mabondia wote 16 wakawepo mazoezini.

Lemmy alisema kwa sasa timu hiyo itafanya mazoezi katika uwanja wa ndani hadi hapo itakapofika programu ya kwenda ufukweni na baadaye gym.
“Kufikia Jumatatu tunatarajia mabondia wote watakuwa wamewasili mazoezini na tutaendelea kufanya mazoezi katika uwanja wa ndani hadi hapo tutakapofikia wakati wa kujenga nguvu kwa mabondia pamoja na viungo, ambapo tutalazimika kuhamia katika fukwe na gym,” alisema Lemmy.

No comments:

Post a Comment