Pages

Friday, May 10, 2013

KWA NINI HISA ZA MANCHESTER UNITED ZILISHUKA ASILIMIA 5%?


Taarifa za kustaafu kwa kocha wa Manchester United, Sir Alex Fergusonzimeifanya klabu hiyo kupoteza mapato yake.
Huku maelfu wa mashabiki wakionekana kushtushwa na habari za kustaafu kwa Fergie maarufu kama babu, lakini pia upande wa masoko kwa klabu ya Manchester United kumekuwa na pigo pia.
Wachambuzi wa masuala ya biashara wameeleza hofu yao juu ya kushuka kwa biashara za United kufuatia kuondoka kwa Ferguson kwa kusema itakuwa kazi kubwa kumpata mrithi wake ambaye ataweza kuchagiza mafanikio ya klabu hiyo yatakayovutia wadhamini mbalimbali kama alivyofanya kwa miaka 27 aliyokaa na United.Hii ni baada ya kushuka kwa ununuzi wa hisa za klabu hiyo kwa zaidi ya asilimia tano kwenye soko la hisa la New York. 

Familia ya Malcom Glazer yenye makao yake Miami nchini Marekani ambayo ndio inayomiliki klabu ya Manchester United bado haijatangaza mrithi wa Ferguson japo wadadisi na vyanzo vya karibu vya United vinasema huenda kocha wa Everton, David Moyes akakabidhiwa jukumu la kuifundisha United,taarifa ambazo hazijathibitishwa wala kukanushwa na uongozi wa Old Trafford.
Kushuka huko kwa hisa za United kumeifanya klabu hiyo kupoteza mapato yake kwa karibu asilimia 1.3 kwa hisa moja ambayo hununuliwa kwa dola za kimarekani 18.52 kwa hisa.

Licha ya kushuka kwa hisa hizo kufuatia taarifa za kustaafu kwa Ferguson lakini zaidi ya asilimia 30 ya hisa za United ziliuzwa kwenye soko la hisa hii leo.

No comments:

Post a Comment