Pages

Friday, May 10, 2013

KOCHA MPYA WA UNITED DAVID MOYES KUANZA MECHI YAKE YA KWANZA YA MASHINDANO DHIDI YA MACHESTER CITY


Kocha mpya wa Manchester United, David Moyes mwenye umri wa miaka 50, atajiunga rasmi na klabu yake hiyo mpya Julai Mosi na kuanza kazi. 

Moyes aliyesaini mkataba wa miaka sita kuifundisha Manchester United baada ya kujiuzulu kwa Alex Ferguson, mechi yake ya kwanza ya mashinda itakuwa kati ya wapinzani wakubwa wa Man United, Manchester City au Wigan.

Mechi hiyo itachezwa Agosti 11 kwenye Uwanja Wembley jijini wakati wa mchezo wa ngao ya jamii.
Akizungumza kwa mara ya kwanza baada ya kuingia mkataba huo wa miaka sita kuchukua nafasi hiyo ‘nzito’ ya Ferguson, Moyes alisema: “Ni heshima kubwa kuchaguliwa kushika nafasi ya Ferguson, ninaamini atakuwa amnipendekeza kuwa hapa.

“Nina heshima kubwa na alichofanya katika soka kama kocha. Nasikia raha kuchukua nafasi baada ya kocha bora kabisa duniani, lakini pia bahati ya kuinoa klabu kubwa kama Manchester United. Nina matumaini makubwa ya kufanya vizuri.”

“Nawashukuru sana Everton ambao nimefanya nao kazi kwa muda mrefu sana na wamekuwa watu wazuri na waliochangia mafanikio yangu hadi kufikia hapa nilipo, nawashukuru sana.”

Mechi dhidi ya Manchester City kama wakiwa mabingwa wa FA itakuwa ni mtihani mgumu kwa Moyes ambaye atakuwa ametoka katika mechi za maandalizi kujiandaa na msimu mpya na tayari atakuwa ameingoza timu hiyo katika mechi za kujipima nguvu na kuandaa kikosi.

No comments:

Post a Comment