Pages

Wednesday, May 22, 2013

SIMBA YAMNASA BEKI WA AZAM FC, SAID MORAD


SIMBA ipo kwenye hatua nzuri ya kumrejesha beki wake wa zamani, Said Morad, aliyekuwa akikipiga katika kikosi cha Azam FC.

Beki huyo wa kati, Morad, ambaye alikumbukwa na kashfa ya rushwa katika klabu yake ya Azam, yupo kwenye rada za Simba na kwamba huenda akarudi kuzivaa jezi za rangi nyekundu na nyeupe msimu ujao.

Morad alikumbwa na kashfa nzito pamoja na wakali wengine wa Azam akiwamo Erasto Nyoni, Aggrey Morris na Deo Munishi 'Dida', kwamba walituhumiwa kupokea rushwa ili kucheza chini ya kiwango katika mechi ya mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara zilizofanyika msimu huu.

Lakini, Takukuru iliwasafisha nyota hao na kuweza kurudi kuichezea timu yao katika mechi za kumalizia msimu, ambapo Yanga ilitoka kidedea kwa kunyakua ubingwa.
Habari  zilizopo zinabainisha kwamba Simba ilifanya mazungumzo na beki huyo kwa ajili ya kuinasa huduma yake msimu ujao.

Morad aliwahi kuichezea Simba kabla ya kutimkia Kagera Sugar, ambapo pia alihama na kujiunga na Azam FC.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zakharia Hanspope, alikataa kuzungumzia suala la usajili beki huyo kwa madai kwamba masuala yote ya usajili yatafanywa baada ya kupata ripoti ya kocha wao, Patrick Liewig mwishoni mwa wiki hii.

No comments:

Post a Comment