Pages

Thursday, April 25, 2013

YANGA YAMPA MKATABA KASEJA



PAMBANO la watani wa jadi Simba na Yanga, limeonekana kuwabakisha Kipa, Juma Kaseja na beki wa kulia wa timu hiyo, Nassoro Masoud 'Chollo' katika usajili ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kaseja na Chollo ni kati ya wachezaji wanaotarajiwa kuongezewa mikataba mipya kabla ya mechi yao, itakayochezwa Mei 18, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Habari zilizopatikana Dar es Salaam jana, zilielezwa kwamba uongozi wa klabu hiyo, umeanza kuandaa mikataba ya wachezaji wote ambao wataendelea kuitumikia timu hiyo.

 Chanzo hicho kilieleza kwamba, mikataba ya wachezaji hao itakamilika kabla ya mechi hiyo, ili waweze kucheza wakiwa na matumaini mapya ya kuendelea kuichezea timu hiyo, lakini kikubwa ni kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo huo.

Kilieleza matarajio ya uongozi huo ni kutaka kumalizana na wachezaji wote ambao mikataba yao imemalizika ili wabakie na wale wapya watakaosajiliwa kuanzia msimu ujao.
Wakati huo huo, Ofisa Habari wa Klabu hiyo, Ezekiel Kamwaga alikiri kuwepo kwa mazungumzo  ya mwisho ya wachezaji ambao wataendelea nao msimu ujao.

Kamwaga alisema wachezaji hao wanatarajia kupewa mikataba mipya kabla ya mechi yao dhidi ya Yanga, kutokana na wapo katika hatua ya mwisho ya kukamilisha makubaliano yao.
"Tumeanza kuzungumza na baadhi ya wachezaji ambao tuna imani tutaendelea nao msimu ujao na wenyewe wanajijua," alisema Kamwaga.

Baadhi ya wachezaji wanaotarajia kumaliza mikataba yao ni Amir Maftah, Felix Sunzu, Amri Kiemba, Shamte Ally, Chollo na Kaseja.
Kutokana na hali hiyo tayari Kaseja alikuwa ameanza kufanya mazungumzo na baadhi ya klabu nchini ikiwemo klabu ya Ashanti United ya jijini Dar es Salaam, ambayo ilionyesha nia ya kumsajili.

No comments:

Post a Comment