Pages

Monday, April 29, 2013

WEBB KUCHEZESHA MADRID vs DORTMUND


NYON, Uswiss
SHIRIKISHO la Soka Ulaya (UEFA), limemteua mwamuzi wa Kiingereza, Howard Webb kuchezesha pambano la nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Real Madrid na Borussia Dortmund, kesho kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu.

Real Madrid wakiwa nyumbani wanahitaji kuwa kwenye kiwango cha juu ilikuweza kurudisha mabao 4-1 waliyofungwa kwenye mechi ya kwanza, hii inamaanisha kwamba, Webb atakuwa na kazi ya ziada hiyo kesho.

Webb amewahi kuchezesha mechi ya fainali ya Kombe la Dunia 2010 nchini Afrika Kusini, kati ya Hispania na Uholanzi, pia mwaka huo huo alichezesha pambano la fainali ya ligi ya mabingwa kati ya Bayern Munich na Inter Milan.

Kwenye fainali ya Kombe la Dunia, Webb alipondwa kutokana na kushindwa kumpa kadi nyekundu, Nigel de Jong baada ya kumrukia kifuani Xavi Alonso.

No comments:

Post a Comment