Pages

Monday, April 29, 2013

LEWANDOWSKI: PEPE ALINIOMBA NIWAONEE HURUMA



DORTMUND, Ujerumani
MSHAMBULIAJI wa Borussia Dortmund, Robert Lewandowski ametoboa siri kwamba beki wa Real Madrid, Pepe alimfuata na kumwambia mabao aliyofunga yanatosha wakati wa pambano baina ya timu hizo ambalo Dortmund walishinda kwa mabao 4-1.

Lewandowski ambaye alifunga mabao yote manne ya Dortmund kwenye mechi hiyo, alisimulia jinsi ambavyo Pepe alimfuata na kumwambia awakaushie, kwa sababu mabao manne aliyofunga yanatosha.

“Wakati tukipiga moja ya kona za mwisho mwisho, Pepe alinifuata na kuniambia, umefunga mabao manne tayari, hudhani kama hayo yanatosha?” Alisema Lewandowski.

“Kila goli lilikuwa tofauti. La kwanza lilikuwa pande safi la Mario Gotze nilimtoroka Pepe na kuweka mpira mguuni, bao la pili nijua kuwa sijaotea, la tatu lilikuwa bora zaidi kwangu, penalti sina cha kuongea katika hilo.”

No comments:

Post a Comment