Pages

Monday, April 29, 2013

MESSI AWEKA REKODI NYINGINE


Magic: Messi skips past three defenders on the edge of the box (above) before scoring (below)
BARCELONA, Hispania
LIONEL Messi ameweka rekodi nyingine kwenye La Liga msimu huu, safari hii ni rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi ugenini, baada ya kufunga bao lake la 24 ugenini, ndani ya msimu mmoja.

Messi aliingia kutokea benchi kwenye pambano dhidi ya Athletic Bilbao na kuifungia bao la kusawazisha Barcelona kabla ya kumtengenezea Alexis Sanchez na kufanya matokeo kuwa 2-1, lakini Bilbao walichomoa katika dakika za mwisho na pambano hilo lilimalizika kwa sare ya 2-2.

Kwa bao hilo Messi amefikisha mabao 44 ya La Liga msimu huu, huku akiweka rekodi ya kufunga mabao 24 ugenini, na kuvunja rekodi ya Cristiano Ronaldo, aliyoiweka msimu wa 2011/12.

Bao hilo lilikuwa ni bao la 100 la Messi kwenye ligi akiwa na Barcelona. Baada ya kuingia uwanjani kwenye pambano la juzi Messi alionekana kurudia kiwango chake cha kawaida na kumaliza ukame wake wa mechi mbili bila bao.

No comments:

Post a Comment