Pages

Friday, April 26, 2013

POLISI ZANZIBAR YASHIKA NAFASI YA TATU MASHINDANO YA MUUNGANO YA MCHEZO WA WAVU

Mchezaji Burhan Ally wa Polisi Zazibar(blue) akirudisha mpira kwa upande wa Twalipo kwenye mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa mashindano ya Muungano

Mchezaji wa Polisi Zanzibar Shukuru Alli (blue) akipiga mpira huku wachezaji wa Twalipo Faustan Lugenge wakizuia wakati wamchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa mchezo wa wavu wa Mashindano Muungano yaliyofanyika Uwanja wa ndani wa Taifa, Dar es Salaam, Polisi ilishinda na kushika nafasi ya tatu

Wachezaji wa Twlipo wakimsikiliza kocha wakati wa mapumziko

Wachezaji wa Polisi Zanzibar wkisikiliza kocha wao Haji Uzia Vuai (aliyevaa kofia) wakati wa mapumziko


Wachezaji wakitapeana fair play baada ya mchezo

TIMU ya mpira wa kikapu ya Polisi Zanzibar leo imeshika nafasi ya tatu kwenye mashindano ya Muungano yaliyokuwa yanafanyika kwenye uwanja wa ndani wa Taifa kwa kuifunga Twalipo ya Dar es Salaam.

Mchezo huo ambao ulikuwa wa ushindani ulichezwa majira ya asubuhi jana ulishuhudia Polisi Zanzibar ikiongoza kwa seti na kufanya kushika nafasi ya  tatu.
Kwenye seti ya kwanza Polisi walongoza kwa seti 25 kwa 22, seti ya pili 25 kwa 22 na seti ya tatu iliongoza tena kwa seti 31 kwa 29 za Twalipo Dar es Salaam.

Akizungumza jijini, kocha wa timu ya Polisi , Haji Uzia Vuai alisema anashukuru kwa nafasi waliyoshika kwani mashindano yalikuwa magumu kutokana na timu kuajiandaa vema ili wao hawakuwa na maandalizi kutokana na kubanwa na kazi.

“Sisi hatukufanya maandalizi yoyote ila tulikuja kushiriki kwani Muungano ni wetu sote hivyo nafasi tuliyoshika si haba kwa inabidi tukajiandae vema ili mwakani tufanye vema zaidi”, alisema Vuai.

Naye nahodha wa Twalipo, Talib Mohamed alisema wamepoteza mchezo kutokana kuzidiwa ujanja na wapinzani wao na kutumia vema nafasi walizozipata hivyo ni changamoto kwao kujiandae vema kwa mashindano yajayo.

Mashindano ya kikapu yanafanyika kuuenzi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambazo ziliungana Aprili 26, 1964 na kuzaliwa Tanzania

No comments:

Post a Comment