Pages

Friday, April 26, 2013

SIKINDE KUTUMBUIZA MEI MOSI MBEYA NA KUFANYA SHOO TUNDUMA NAUKUMBI BENJAMIN MKAPA

Waimbaji wa Mlimani Park 'Sikinde' Hassani Kunyata, Abdallah Hemba na Hassani Bitchuka

 
BENDI kongwe ya muziki wa dansi nchini, Mlimani Park 'Sikinde' inatarajiwa kutambulisha nyimbo zake mpya katika miji kadhaa wakati wakielekea Mbeya katika sherehe za Mei Mosi.
Sikinde imealikwa kutumbuiza katika sherehe hizo ambazo kitaifa zitafanyikia kwenye mkoa huo wa Mbeya wiki ijayo.

Akizungumza na BINGWA, Katibu wa bendi hiyo, Hamis Milambo alisema  wakiwa njiani kuelekea Mbeya watafanya maonyesho kadhaa katika maeneo mbalimbali ndani ya mkoa wa Mbeya na nje mkoahuo.
Milambo alisema maonyesho hayo yataanza kesho Ijumaa watakapotambulisha nyimbo zao kwenye ukumbi wa Comfort Chamazi na jumamosi wakuwa City Pub uliopo Mwanjelwa.

Siku ya jumapili watatumbuiza Tunduma kabla ya siku ya Mei Mosi kutumbuiza kwenye sherehe za Mei mosi asubuhi kwenye Uwanja wa Sokoine na usiku watakuwa na shoo kubwa kwenye ukumbi wa Benjamini Mkapa Mbeya.


"Siku ya Mei Mosi tukishatumbuiza Uwanja wa Sokoine tutafanya onyesho katika ukumbi maarufu wa Benjamin Mkapa  na kuanza kuanza safari ya kurejea Dar kuendelea na mengine," alisema Milambo.


Milambo anasema katika maonyesho yote watatambulisha nyimbo zao wanazoziandaa kwa ajili ya albamu mpya ya ambazo ni  'Jinamizi la Talaka', 'Kuvunjika kwa Dole Gumba', 'Nundule' na nyingine pia tutawapa burudani ya nyimbo za zilizoifanya Sikinde kutambuliwa kama mabingwa wa Muziki wa Dansi Tanzania.


No comments:

Post a Comment