Pages

Friday, April 26, 2013

KING KIKII, MSONDO NGOMA NA KHADIJA KOPA JUKWAA MOJA SHEKINAH GARDEN.


Kundi zima la Capital Wazee Sugu wakiwa chini ya bwana mkubwa Kikumbi Mwanza Mpango King Kikii watasahambulia ndani ya ukumbi wa Shekinah Garden mbezi makonde inayotazamana na kituo cha mafuta cha Engen ijumaa ya tarehe tatu mwezi wa tano mwaka huu (03/05/2013).
Akiongea na gazeti hili, afisa masoko wa kampuni ya D & I Entertainment Peter Mwendapole amesema mbali ya King Kikii, pia usiku huo watashambulia jukwaa moja na magwiji wa muziki wa dansi nchini Msondo Ngoma Music Band ” baba ya muziki” ambao siku hiyo watamtambulisha kwa mashabiki wao mwanamuziki mkongwe mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni Shaaban Dede mwana aliyerejea nyumbani. 

Aidha Mwendapole amesema ili kuikamilisha burudani hii ya aina yake na inayofanyika kwa mara ya kwanza ndani ya Shekinah Garden mbezi makonde, malkia wa mipasho Afrika Mashariki na Kati Bi Khadija Omar Kopa naye atawakonga mashabiki watakaofika kwa miondoko yake ya taarabu na hasa kibao chake kinachotamba hivi sasa cha mjini chuo kikuu.

Mwendapole amewataka mashabiki kufika kwa wingi kwani hii ni buruda ni ya aina yake ambayo itakuwa na vionjo vya kila aina, na kila atakayefika atafurahi kwani makundi yote haya yatatumbuiza kwa utaratibu maalum ili kila mmoja atii kiu yake.

Kuhusu ulinzi na usalama, amesema yote hayo yameimarishwa

No comments:

Post a Comment