Pages

Sunday, April 7, 2013

MANCHESTER UNITED VS CITY NANI KUCHEKA LEO? OLD TRAFORD PATAWAKA MOTO SAA 4 USIKU


Uso kwa Uso: 
-Ushindi wa Bao 6-1 wa Man City Msimu uliopita ndio kipigo kikubwa kabisa ambacho Man United wamepata katika Ligi Kuu na ilikuwa mara ya kwanza kufungwa Old Trafford Bao 6 tangu Mwaka 1930.
-Hii itakuwa Dabi ya Manchester ya 165 na Man United wameshinda mara 69, Man City mara 45 na Sare 50.
-Sir Alex Ferguson na Roberto Mancini watakutana kwa mara ya 11 kama Mameneja na Ferguson ameshinda Mechi 6 na Mancini Mechi 4.

Ushindi kwa Man United kwenye Mechi hii utawafanya wawe Pointi 18 mbele ya Man City na watakuwa wanahitaji Pointi 4 tu katika Mechi 7 zitakazobaki ili wawe Mabingwa.
Endapo wataibuka Mabingwa, Ubingwa huo utakuwa wa 20 katika Historia ya Man United na utakuwa ni Ubingwa wa 13 chini ya Meneja wao Sir Alex Ferguson ndani ya Miaka 21 ya Ligi Kuu.

Kwa Meneja wa Man City, Roberto Mancini, kushinda au kufungwa Old Trafford, hakutabadilisha ukweli kuwa Msimu huu umekuwa ni wa kuvunja moyo kwao hasa baada ya Msimu uliopita kutwaa Ubingwa wao wa kwanza baada ya Miaka 44.


Lakini, hata hivyo, bado wapo kwenye FA CUP na Wikiendi ijayo wapo Wembley kucheza Nusu Fainali dhidi ya Chelsea.
Mwenyewe Mancini amekiri hali hii pale alipotamka: “Nimesema mara nyingi sisi ni Timu changa. Ni Miaka miwili tu tumeanza kugombea Ubingwa. Tunataka kutwaa nafasi ya Pili kwenye Ligi, tuna Mechi na United, kisha ugenini na Tottenham, ipo Nusu Fainali ya FA CUP! Wiki mbili zijazo ni muhimu kwetu!”


MATOKEO MECHI ZA HIVI KARIBUNI:
 
9 Desemba 2012: Man City 2 Man United 3 [BPL-2012/13]
30 Aprili 2012: Man City 1 Man United 0 [BPL-2011/12]
8 Januari 2012: Man City 2 Man United 3 [FA CUP]
23 Oktoba 2011: Man United 1 Man City 6 [BPL-2011/12]
7 Agosti 2011: Man United 3 Man City 2 [NGAO ya HISANI]


RATIBA/MATOKEO
Jumapili 7 April
[Saa 9 na Nusu Mchana] 
Liverpool 0 v West Ham 0

[Saa 10 Dak 5 Jioni] 
Tottenham 2 v Everton 2
[Saa 11 Jioni] 
Chelsea 2 v Sunderland 1
Newcastle 1Vv Fulham 0
[Saa 12 Dak 10 Jioni] 
QPR 1 v Wigan 1

Leo Jumatatu 8 Aprili 
[Saa 4 Usiku] 
Man United v Man City

No comments:

Post a Comment