Pages

Monday, April 8, 2013

AHMED KARAMA DIWANI WA BWILINGU BAGAMOYO, PWANI AAHIDI MAKUBWA KWENYE NGUMI


Diwani wa Kata ya Bwilingu Chalinze Bagamoyo, Ahmed Karama Nassar
Bondia Martin Shekivuli kushoto akipambana na Abdull Ndosa wakati wa mpambano wao wa kirafiki uliochezwa jana mpambano huo ulitoka droo

Bondia Amour Mzungu katikati akipambana na Josefu Marwa wakati wa mpambano wao wa kirafiki uliofanyika jana kushoto ni refarii Ibrahimu Kamwe
Refarii Ibrahimu Kamwe akimnyoosha mkono juu Amour Mzungu kuwa mshindi wa mpambano huo dhidi ya Josefu Marwa 
Diwani wa Kata ya Bwilingu Chalinze Bagamoyo,Ahmed Karama Nassar katikati akizungumza mbele ya mabondia Issa Omari kushoto na Shabani Madilu kabla ya mpambano
Diwani wa Kata ya Bwilingu Chalinze Bagamoyo,Ahmed Karama Nassar, amekubali kushirikiana na wadau wa mchezo wa ngumi waweze kupata ukumbi maalumu wa mchezo huo.

Chalinze ambaye alikuwa mgeni rasmi alitoa kauli hiyo jana kwenye mapambano ya ngumi uliopigwa katika ukumbi wa CCM Mwijuma, Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.

“Nitarajia kuuletea maendeleo mchezo huu kwa kuwa mmenishawishi kuupenda japo wadhamini wachache ndio wanaojitokeza”, alisema Karama.

Pia alisema  ameandaa mpambano utakaochezwa Chalinze kwa ajili ya kuhamasisha mchezo huo April 21, mwaka huu na kuwaomba wadau wote wa ngumi wafike Chalinze, wasaidie kuhamasisha mchezo huu

Kwenye pambano hilo mabondia toka Dar es Salaam ambao watapambana na mabondia wa Chalinze hivyo kutakuwa na ushindani mkubwa na ameahidi usafiri wa kuwapeleka Chalinze mabondia na mashabiki watakaopenda kwenda.

Karama kwa kudhihirisha kuwa amepania kuendeleza ndondi alitoa pesa taslimu shilingi 1,500,000 kwa ajili ya malipo ya baadhi ya mabondia waliokuwa hawajilipwa na kuanza kudai kugoma kupanda ulingoni juzi.

Mdau wa ngumi Ibrahimu Kamwe amempongeza Karama na kuomba watu na viongozi wengine waige mfano wake na kuahidi hata Chalinze atakwenda kushuhudia pambano hilo

No comments:

Post a Comment