Pages

Thursday, April 25, 2013

MAJERUHI WA YANGA WAREJEA UWANJANI, KAZI MOJA TU MEI MOSI



KIKOSI cha timu ya soka ya Yanga, sasa kimekamilika kwa asilimia 100 baada ya wachezaji wao waliokumbwa na majeruhi kuanza mazoezi kujiandaa na mechi yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union, itakayochezwa Mei Mosi, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts alipandwa na presha kutokana na wachezaji wake wengi kukumbwa na majeruhi wakiwa katika wakati mgumu wa kuwania ubingwa wa ligi hiyo.

Wachezaji ambao walikuwa majeruhi ni Jeryson Tegete, Juma Abdul, Khamis Kiiza na Haruna Niyonzima ambao tayari wamerejea kikosini, huku Didier Kavumbagu na Ladislaus Mbogo wakianza mazoezi mepesi.

 Akizungumza jijini,, Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh alisema wachezaji hao walianza mazoezi jana kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam.

Saleh alisema, Kavumbagu alikuwa anasumbuliwa kifundo cha mguu na Mbogo alikuwa anauguza kidonda baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo katika shavu lake.

 “Ni jambo la kushukuru kwa kuwa wachezaji hao walikuwa ni majeruhi kwa muda mrefu, hivyo sasa wameanza mazoezi,” alisema Saleh.

No comments:

Post a Comment