Pages

Friday, April 26, 2013

JESHI STARS WASHINDWA KUFUTA UTEJA KWA MAGEREZA STARS BAADA YA MAGEREZA KUTWAA UBINGWA WA MUUNGANO KWA MCHEZO WA WAVU

Nahodha wa Magereza Kevin Peter akikabidhiwa kombe na Naibu Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana, Michezo na Utamaduni Juliana Yassoda

Wachezaji wa Magereza wakishangilia na kombe lao


Magereza wakipeana mbinu za kuimaliza jeshi stars




Nahodha wa Jeshi Stars  Magobe akikabidhiwa kombe lao kwa kushika nafasi ya tatu

Mashabiki wakishangilia



Kikosi cha Magereza

Kikosi cha Jeshi Stars
Kaimu Mkurugenzi wa Michezo toka wizara ya Habari, Vijana michezo na Utamaduni akizungumza kabla ya kutoa zawadi


TIMU ya Magereza wanaume ya mchezo wa wavu jana iliendeleza ubabe wake kwa kuifunga Jeshi stars kwa seti 3 kwa mbili kwenye mchezo wa nkusherehekea maaadhimisho ya miaka 49 ya Muungano uliochezwa kwenye uwanja wa ndani wa Taifa.

Mchezo huo ulikuwa wa ushindani kwa Magereza ambaye ndie alikuwa bingwa mtetezi alimaliza seti ya kwanza akiwa amefungwa 25 kwa 15 hali iliyowafanya kujiuliza  na kuanza kubadilika kila seti
Seti ya pili ilimalizika kwa jeshi Stars kuongoza kwa 25 kwa 23  na seti ya tatu Magereza walimaliza wakiwa na 25 dhidi ya 22 za Jeshi Stars.

Kwenye seti ya tatu Magereza waliendelea kushika usukani baada ya kuifunga tena Jeshi Stars kwa 25 dhidi ya 22, kulazimika kuongezwa seti nyingine ya kutafuta bingwa.

Seti ya mwisho ilikuwa ngumu kwa kila timu ilijitahidi kuhakikisha inamaliza mshindi lakini Magereza ndio ilifanikiwa kumaliza wakiwa 16 dhidi ya 14 za Jeshi Stars na kuwafanya waendelee kuwa wateja wa Magereza.

Mchezo huu ulilazimik kusimama kila saa kutokana na wachezaji kulalamikia maamuzi ya refa.
Zawadi za wachezaji bora zilikwenda kwa Athuman Rupia na Nassor Sharifu wa Jeshi Stars ambao kila mmoja alipewa zawadi ya mpira mmoja na wa tatu alikuwa Kevin peter wa Magereza ambaye naye pia alipewa zawadi ya mpira mmoja.
Pia kila timu iliyoshiriki ilipewa mipira mitano mitano.







No comments:

Post a Comment