Kaimu Mkurugenzi wa Michezo toka wizara ya Habari, Vijana michezo na Utamaduni akizungumza kabla ya kutoa zawadi
TIMU ya
Magereza wanaume ya mchezo wa wavu jana iliendeleza ubabe wake kwa kuifunga
Jeshi stars kwa seti 3 kwa mbili kwenye mchezo wa nkusherehekea maaadhimisho ya
miaka 49 ya Muungano uliochezwa kwenye uwanja wa ndani wa Taifa.
Mchezo huo ulikuwa wa ushindani kwa Magereza ambaye ndie
alikuwa bingwa mtetezi alimaliza seti ya kwanza akiwa amefungwa 25 kwa 15 hali
iliyowafanya kujiuliza na kuanza
kubadilika kila seti
Seti ya pili ilimalizika kwa jeshi Stars kuongoza kwa 25 kwa
23 na seti ya tatu Magereza walimaliza
wakiwa na 25 dhidi ya 22 za Jeshi Stars.
Kwenye seti ya tatu Magereza waliendelea kushika usukani
baada ya kuifunga tena Jeshi Stars kwa 25 dhidi ya 22, kulazimika kuongezwa
seti nyingine ya kutafuta bingwa.
Seti ya mwisho ilikuwa ngumu kwa kila timu ilijitahidi
kuhakikisha inamaliza mshindi lakini Magereza ndio ilifanikiwa kumaliza wakiwa
16 dhidi ya 14 za Jeshi Stars na kuwafanya waendelee kuwa wateja wa Magereza.
Mchezo huu ulilazimik kusimama kila saa kutokana na wachezaji
kulalamikia maamuzi ya refa.
Zawadi za wachezaji bora zilikwenda kwa Athuman Rupia na
Nassor Sharifu wa Jeshi Stars ambao kila mmoja alipewa zawadi ya mpira mmoja na
wa tatu alikuwa Kevin peter wa Magereza ambaye naye pia alipewa zawadi ya mpira
mmoja.
Pia kila timu iliyoshiriki ilipewa mipira mitano mitano.
|
No comments:
Post a Comment