Pages

Friday, April 26, 2013

FAINALI ZA MISS UTALII TANZANIA 2013 KUFANYIKA TANGA SERIKALI YATOA KIBALI



Baada ya kukwama kwa Muda Mrefu Kutokana na baadhi ya wadhamini kushindwa kutimiza ahadi zao za udhamini hatimaye Bodi ya Mashindano ya Miss Utalii Tanzania imehamishia fainali hizi za Miss Utalii Tanzania 2012/13 mkoani Tanga badala ya Dar es salaam ambazo zilikuwa zifanyike awali.

Taratibu zote za fainali za Show ya Taifa kufanyika Tanga zimekamilika ikiwemo kukamilisha  sheria  ya  ya uendeshaji wa Shughuli za sanaa na Fainali za Urembo ambapo Serikali kupitia Baraza la Sanaa la Taifa hatimae limetoa kibali kwa fainali hizo Kufanyia Tanga tarehe 11.05.2013, waandaaji wamewasilisha BASATA uthibitisho wa Zawadi kwa Washindi, Pamoja na mikataba ya kulinda haki na wajibu wa waandaaji na washiriki wa Fainali Hizo.

Hii itakuwa ni Mara ya kwanza kwa Mkoa wa Tanga kuwa wenyeji wa Fainali za Taifa za mashindano ya Urembo na ni mara ya pili kwa Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania Kufanyikia Nje ya Dar es salaam baada ya Fainali za mwaka 2005 kufanyikia Mkoani Arusha.

Hii ni Heshima na Fulsa ya pekee kwa Mkoa wa Tanga ya kuhidhilishia na kuutangazia Ulimwengu vivutio vyake vya Utalii, Utamaduni, Uwekezaji, na Miundo mbinu kitaifa na kimataifa. Lakini pia hii ni Fulsa kwa Jiji la Tanga kuuthibitishia Ulimwengu kuwa Jiji la Tanga linao uwezo wa kuwa wenyeji wa Tukio la Kitaifa. Kufanyika kwa Shindano hili Mkoani Tanga kutasaidia pia Kuhamasisha pia Kampeni dhidiya , Uharibifu wa mazingira, Uvuvi Haramu, Uwindaji Haramu, Tohara kwa wanawake, Utamaduni, mila na Desturi kongwe na Potofu.Madawa ya kulevya, Rushwa, Ubaguzi wa Kijinsia, na Mmomonyoko wa Maadili katika jamii.

Wakati huo serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imewapongeza juhudi zinazo fanywana Waandaaji wa Miss Utalii Tanzania  za kutangaza vivutio vya utalii na utamaduni wa Tanzania kitaifa na kimataifa kwa kuipatia Sifa kubwa Tanzania kupitia mashindano hayo. 

Kwa mujibu wa maelezo ya Barua ya Tarehe 19.04.2013 iliyo sainiwa na Ndugu Z. A Kimwaga kwa niaba ya Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwenda kwa waandaaji wa Miss Utalii Tanzania. Wizara na serikali kwa ujumla inatambua juhudi zinazofanywa na waandaaji wa mashindano haya katika kukuza utalii wa ndani na Utalii wa Kitamaduni.

Katika kuthibitisha hilo Wizara imewashauri waandaaji wa mashindano hayo kuwaslisha maoombi ya msaada kutoka serikalini kwa wakati na kwa kuzingatia misimu na Bajeti ta serikali ili kuwe na uwezekano wa serikali Kudhamini mashindano hayo. Hata hivyo Serikali kupitia Taasisi zake za Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa(TANAPA) , Mamlaka ya Ngorongoro(NCIA), na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa miaka yote ikiwepo mwaka huu imekuwa ikitoa udhamini wa Hali na Mali katika kufanikisha Mashindano hayo.

Nae Rais wa Mashindano hayo Gidion Chipungahelo kwa niaba ya Bodi ya Mashindano amewaomba Radhi watanzania wote , wadau w ashindano , washiriki, wadhamini na wengine wote walioguswa au kuathiriwa kwa namna yoyote.

No comments:

Post a Comment