Pages

Monday, April 29, 2013

NYOTA WA ARSENAL AWAFAGILIA VIJANA UGANDA



KAMPALA, Uganda
NYOTA wa zamani wa Arsenal na timu ya Taifa ya Cameroon, Lauren Etame Mayer amesema amekuwa na matumaini na vipaji vya vijana wa Uganda na huenda safari yake ya nchini humo ikazaa matunda kwa kuona nyota kadhaa wanachipua katika soka la kulipwa kwenye klabu kubwa nchini Uingereza na barani Ulaya.
Mayer alikuwa nchini Uganda kwa ziara ya kuibua vipaji vya Airtel Rising Stars, ambapo aliongozana na Meneja uhusiano wa klabu ya Arsenal, Luke Wilson, ambapo alisema vipaji alivyoviona vinatia matumaini sana katika soka la Uganda.
“Vijana wana vipaji, wakipata elimu nzuri na kupata mafunzo mazuri katika shule za vipaji, muda si mrefu Uganda itakuwa na wachezaji watakaotamba sana Afrika na duniani,” alisema.
Ziara hiyo ni sehemu ya ushirikaino kati ya klabu ya Arsenal, Airtel na Chama cha soka cha Uganda, ulioanza mwaka 2011 ambao umelenga kuibua vipaji vya vijana. Tayari vijana 1,500 wamechukuwa na wako katika mafunzo kwenye shule maalum, ambako hupata mafunzo na kufanya ziara za kimichezo katika nchi mbalimbali

No comments:

Post a Comment