Pages

Wednesday, April 24, 2013

KIMENUKA TENA LEO HISPANIA BORUSSIA DORTMUND YAICHAPA REAL MADRID 4-1, UEFA CHAMPIONS LEAGUE

Borussia Dortmund wakiikaribisha Real Madrid kwenye Uwanja wao Signal Iduna Park kwenye Mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONSWameanza kwa furaha kwa kuifunga bao la dakika ya 8 kupitia krosi iliyopigwa kama kona na hatimaye kumkuta mchezaji Robert Lewandowski na kuusindikiza hadi nyavuni mwa goli la Real Madrid linalolindwa na kipa wao Diego López.
Robert Lewandowski akishangilia baada ya kufunga bao dakika ya 8
Ronaldo akionekana kusikitika baada ya kufungwa bao la 1.

Dakika ya 43 Cristiano Ronaldo anasawazisha bao na kufanya 1-1 na kipindi cha kwanza kinamalizika. Kipindi cha pili Dakika ya 50 mchezaji Robert Lewandowski akaongezea Real Madrid bao jingine la pili na kufanya 2-1, Huku Real wakibaki wakiduwaa. Ndani ya Dakika tano tu wakafungwa bao jingine kupitia mchezaji huyo huyo Robert Lewandowski mwenye umri wa miaka 24 mchezaji wa Dortmund na timu ya taifa ya Poland akaipatia bao jingine la tatu na kufanya 3-1. Dakika ya 67 Robert Lewandowski akaipatia bao la nne kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa Dortmund kuangushwa eneo hatari na kisha Robert Lewandowski kufunga bao hilo na kufanya 4-1 dhidi ya Real Madrid.
Ronaldo akisawazisha bao hilo na kufanya 1-1

Ronaldo akishangilia 

Tussle: Reus rushes for the ball with Real Madrid defender Pepe
Defender Pepe akijitetea akitaka kumvuta mchezaji wa DortmundCristiano Ronaldo na Mats Hummells wakichuana usiku huu.
The magic number: Lewandowski shows how many goals he's scored after his hat-trick
Mchezaji wa Dortmund Lewandowski akionesha kwa vidole juu baada ya kufunga hat-trick na kuongeza baadaye bao la 4 peke yake!



VIKOSI:
Dortmund: Weidenfeller, Subotic, Hummels, Piszczek (Grosskreutz 82) , Schmelzer, Bender, Gundogan, Reus, Gotze, Lewandowski, Blaszczykowski (Kehl 82)
Subs: Langerak, Leitner, Sahin, Schieber, Santana
Goal: Lewandowski 8, 50, 55, 67

Real Madrid:Diego López, Varane, Pepe, Sergio Ramos, Coentrão, Khedira, Ronaldo, Özil, Xabi Alonso (Kaka 80), Modric (Di Maria 68), Higuaín (Benzema 69)
Subs: Casillas, Albiol, Callejon, Nacho
Goal; Ronaldo 43
Referee: Bjorn Kuipers

RATIBA/MATOKEO
NUSU FAINALI 

Jumanne Aprili 23 
Bayern Munich 4 v Barcelona 0
Jumatano Aprili 24 
Borussia Dortmund 4 v Real Madrid 1
 

MARUDIANO
Jumanne Aprili 30 

Real Madrid v Borussia Dortmund
Jumatano Mei 1 
Barcelona v Bayern Munich

No comments:

Post a Comment