Pages

Friday, April 26, 2013

SASA CHAMA CHA MPIRA WA PETE DUNIA IFNA KUJULIKANA KAMA INF


 
Shirikisho linalosimamia mchezo  wa mpira wa pete duniani  (IFNA) limebadili jina na sasa litajulikana kama  shirikisho la kimataifa la mpira wa pete

Shirikisho hilo lenye makazi yake makuu huko umoja wa nchi za kifalme limesema lipo kwenye kipindi cha mpito katika kuuboresha mchezo huo ambapo kitaongeza mchezo mwingine ujuliakan nao kama Fast5 na michezo mingine ya kimaendeleo

Shirikisho hilo limesema kuwa mabadiliko ya jina hilo kutoka  IFNA hadi  INF ni kuliweka shirikisho hilo kwa ukaribu na vyama vingine vya michezo duniani .

Aidha shirikisho hilo limesema hata nembo ya kampuni hiyo imebadilishwa na nembo ya sasa itakuwa inaashiria uongozi zaidi tofauti na hapo mwanzo na lengo kubwa ni kubadili muonekano wa mpira wa pete.
Katika nembo hiyo ya sasa inaonyesha mikono inayoshikilia mabara yote sita na kuyaleta pamoja katika mchezo wa mpira wa pete  ".
Nembo hiyo mpya itazungushwa katika mabara yote kuashiria kuwa nembo mpya imeanza kufanya kazi .

No comments:

Post a Comment