Pages

Sunday, April 7, 2013

DICKSON MARWA AIBUKA TIGO NUSU MARATHON KARATU,


washiriki wakijiandaa tayari kwajili ya kuanza mashindano wakiwa pamoja na Naibu waziri wa maliasili na utalii Mh, Lazaro Nyalandu pamoja na waandaaji

Mh, Lazaro Nyalandu akimtoka Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mheshimiwa Anthony Mtaka katika mbio hizo

Mwimbaji wa bongoflava Barnaba akiwa na Irene Kiwia manager director kutoka Frontline Porter Novelli ambaye pia alikuwa mshiriki wa miss Tanzania wakishiri mbio hizo ambapo walimaliza mbaka mwisho.


Mshindi wa kwanza kwa upande wa wanawake bi Jacquline Salum toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akiwatoka washiriki wenzie

Bwana Dickson akihojiwa na wandishi wa habari baada ya kushinda mbio hizo

Naibu waziri wa Mali asili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabizi zawadi kwa mshindi wa kwanza bwana Dicksoni Marwa.

Dickson Marwa alijichukulia kitita cha shillingi millioni moja za kitazanzania baada ya kuibuka mshindi wa Tigo Ngorongoro nusu Marathon ambapo mshindi wapili bwana Stephano Huche ambae nae ni aliweza kuondaka na kitita cha shillingi laki tano.

Mashindano haya ambayo lengo lake ni kuhamasisha mapingano dhidi ya ugonjwa wa malaria yameandaliwa na taasisi tanzu ya kujitolea ya kampuni ya Utalii ya ZARA Tanzania Adventures ambayo husaidia shughuli mbalimbali za kijamii kwa kujitolea na kudhaminiwa na kampuni ya Tigo.
Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Waziri wa Maliasili na utalii Lazaro Nyalandu alisema kila hatua moja ambayo atakuwa anakimbia mkimbiaji itakuwa inahamasisha umoja katika kupambana na malaria hatua hiyo pia ni ishara inayoonyesha nia njema ya waandaaji wa mbio hizo kutokana na lengo la kupambana na ugonjwa huo hatari unaoua wananchi wengi 
"Kwa takwimu tulizonazo hadi sasa ni kwamba malaria inaua watu zaidi 888,000 barani Afrika na robo tatu wa watu hao ni watoto wenye umri chini ya miaka mitano na kwa hali hiyo, mbio hizi zinachagiza uhamasishaji wa kupambana na ugonjwa huo" alisema 
Mbio hizo ambazo zinafanyika kila mwaka zimeshirikisha vilabu 26 kutoka Tanzania nzima zilizo na wanariadha 236, zilianzia katika geti la kuingilia kwenye Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kumalizikia katika uwanja wa Karatu mjini. 
Kwa upande wa wanawake, mwanariadha Jacquline Salum toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) aliibuka mshindi na kujinyakulia kitita cha shilingi laki tano, akifuatiwa na Zakia Mrisho aliyejinyakulia shilingi laki tatu. 
akizugumza Mkurugenzi wa Zara Tours Leila Ansell ambao ni waaandaaji wa mashindano hayo alisema mashindano ya Mwaka huu wamepata washiriki wengi zaidi ili kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia kupambana na ugonjwa na Maralia pia ni kuunganisha pamoja watalii na wananchi wa Tanzania pamoja na kukusanya fedha zitakazotumika katika mapambano ya ugonjwa hatari wa Malaria. 


Aidha mashidano hayo yalianza mapema saa 12:00 asubuhi leo kwa mbio za watoto kuazia eneo la Mnadani, Karatu, mbio za wakubwa za km 21 zilianzia geti kuu la Ngorongoro na kumalizikia viwanja vya mazingira bora Karatu.

No comments:

Post a Comment