Pages

Saturday, April 6, 2013

AZAM YAFUZU HATUA YA TATU LICHA YA SARE NA BARRACK YOUNG CONTROLLERS, KOMBE LA SHIRIKISHO, UWANJA WA TAIFA

Kipre Tchetche 


Kipre Tchetche wa Azam FC, akimtoka Prince Jetoh wa Barrack Young Controllers kwenye mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika uliochezwa uwanja wa Taifa leo

AZAM FC imefanikiwa kuingia Raundi ya Tatu ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, licha ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Barack Young Contollers II ya Liberia kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Sare hii katika mchezo wa marudiano wa Raundi ya Pili, Azam imefuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1, baada ya wiki mbili zilizopita kushinda 2-1 mjini Monrovia.
Azam FC sasa itamenyana na timu ya jeshi la Morocco, FAR Rabat wiki mbili zijazo.

Awali mashabiki wengi walivyodhani B.Y.C. ni timu dhaifu lakini timu hiyo iliwachezea wenyeji Azam na kama wangetumia vyema nafasi zao  wangeweza kupata bao.
Pia Azam walipoteza nafasi nyingi za wazi
Kikosi cha Azam FC; Mwadini Ally, Himid Mao, Waziri Salum, Joackins Atudo, David Mwantika, Kipre Balou, Kipre Tchetche, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco ‘Adebayor’, Humphrey Mieno na Brian Umony
Barrack Y.C.; Winston Sayouah, Karleo Anderson, Joseph Broh, Cammue Tummomie, Prince Jetoh, Junior Barshall, Benjamin Gbamy, Abraham Andrews, Randy Dukuly, Mark Paye na Ezekiel Doe.

No comments:

Post a Comment