Pages
▼
Friday, April 5, 2013
KAJALA MASANJA AJICHORA TATOO ILIYOANDIKWA WEMA
Actress Kajala Masanja ambaye hivi karibuni alitolewa mil.13 na Wema Sepetu kama faini yake ili asifungwe ameamua kujichora tattoo yenye jina la Wema kama ishara ya kumshukuru muigzaji huyo.
Kajala amejichora tattoo hiyo mgongoni mwake upande wa kushoto. Hata hivyo baadhi ya watu wakiwemo wasanii wenzake wamemponda kajala kwa uamuzi wake wa kujichora tattoo ya Wema kuwa hakufikiria mara mbili kama kweli alikuwa na nia ya kumshukuru kwa kuwa michoro hiyo kitaalam inadaiwa kuwa na madhara katika ngozi ya mhusika ikiwemo kusababisha kansa.
Pia wamesema hicho ni kitu cha muda tu so Kajala angefikiria mbali zaidi hata baadaye akijaaliwa kupata mtoto mwingine ampe jina la Wema au kitu kingine cha kudumu kuonyesha heshima na shukrani lakini si kujichora tattoo wakidai ni tamaduni za magharibi na ukichukulia issue aliyokuwa nayo mahakamani ilikuwa serious sana.
Actress mmoja aliye karibu na Wema na Kajala kwa sharti la kutotajwa jina lake alisema “cjaona point alofanya Kajala kwa kujichora tattoo, ni kuiga uzungu tu instead angefanya cha maana zaidi hata kumpa mwanae jina la Wema hapo badae”,
Licha ya hayo wengine wamechukulia poa tu kwa alichokifanya Kajala
No comments:
Post a Comment