Pages

Monday, April 8, 2013

MBWANA SAMATTA AIVUSHA TP MAZEMBE SASA KUCHEZA NA ORANDO PIRATES



MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ameiwezesha timu yake ya TP Mazembe kufuzu hatua ya tatu ya Ligi ya Mbingwa barani Afrika baada ya kuifunga Mochudi Centre Chiefs ya Botswana mabao 7-0.
             
Kwenye mchezo wa jana uliochezwa uwanja wa Stade de TP Mazembe mjini Lubumbashi iliibuka na ushindi wa mabao 6-0 na ugenini waliifunga bao 1-0, lililotiwa kimiani na Mbwana Samatta.

Kwenye mchezo wa juzi Samatta ambaye pia ni mshambualiaji wa Timu ya Taifa ‘Taifa Stars alifunga bao kipindi cha pili dakika ya 75 huku mabao mengine yakifungwa na Rainford Kalaba dakika ya sita na 35, Tresor Mputu dakika ya 15 na 80 na msumari wa mwisho ulipigiliwa na Eric Nkulukuta dakika ya 90.

TP Mazembe kwenye mchezo ujao watacheza na Orlando Pirates  ya Afrika ya Kusini ambayo imeisukuma nje Zanaco ya Zambia baada ya kuifunga mabao 3-1ambapo ugenini ilishinda 1-0 na nyumbani juzi ilishinda 2-1.

Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu licha ya kuwa tegemeo kwa timu yao ya TP Mazembe pia nchi yao inawategemea katika kampeni za kufuzu kwenda Brazili 2014, Kombe la Dunia.

No comments:

Post a Comment