Pages

Sunday, March 31, 2013

RAFA BENITEZ KAWAWEKA NJE LUIZ NA COLE NA KUPOKEA KICHAPO



Rafael Benitez amejitetea juu ya maamuzi yake ya kufanya mabadiliko kwa wachezaji saba katika mchezo wa jana ambao Chelsea ilichapwa bao 2-1 na Southampton wakati huu ambapo wanaelekea katika mchezo wao wa robo fainali ya michuano ya FA hapo kesho jumatatu dhidi ya Manchester United.

Walinzi wa David Luiz na Ashley Cole pamoja na kiungo Eden Hazard hawakuwepo katika kikosi ambacho kiliishuhudia hapo jana Chelsea ikidondoka kutoka katika nafasi ya tatu mpaka ya nne ya msimamo wa ligi kuu ya soka England.

Amenukuliwa bosi huyo wa muda akisema "tumefanya hivyo ili kuelewa kikosi na kukijenga"

"Hatukuwa na namna nyingine ya kufanya katika baadhi ya nafasi, tulikuwa na wachezaji hao tuliokuwa nao"

Gary Cahill hakuwepo katika mchezo huo dhidi ya Southampton kwasababu ya maumivu ya mguu kama ilivyokuwa kwa Juan Mata ambaye naye alikuwa ni mgonjwa.

Benitez amesema "lazima tukabiliane na hali katika kila mchezo ni jambo muhimu sana na tulidhani kwa kuwatumia wachezaji hao mambo yangekuwa mazuri"

Licha ya kwamba huo ulikuwa ni mchezo wa tatu mfululizo kwa Chelsea kufungwa ugenini katika ligi ambao umewapandisha juu Tottenham, bosi huyo mhispania amesisitiza kuwa kikosi chake kilikuwa vizuri.


 MICHEZO MUHIMU KWA CHELSEA


1 April: H v Man Utd (FA Cup quarter-final replay)

4 April: H v Rubin Kazan (Europa League quarter-final first leg)

7 April: H v Sunderland (league)

11 April: A v Rubin Kazan (Europa League quarter-final second leg)

No comments:

Post a Comment