Pages

Sunday, March 31, 2013

SIMBA YATOKA SARE NA SHINYANGA UNITED LEO


 SIMBA leo imetoka sare ya kufungana bao 1-1 na Shinyanga United kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga baada ya jana kulazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Toto African kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara

Simba ilicheza mechi hiyo, ili kuendelea kuwapa uzoefu wachezaji wake chipukizi, inaowatumia kwa sasa kwenye Ligi Kuu, baada ya kuwapiga chini baadhi ya nyota wa kikosi cha kwanza kwa utovu wa nidhamu.

Miongoni mwa wachezaji walioachwa kutumikwa na kocha ni Juma Nyosso, Haruna Moshi ‘Boban’, Amir Maftah, Ramadhani Chombo ‘Redondo’, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Komabil Keita, Abdallah Juma na Paul Ngalema.

Katika mchezo wa leo, bao la Simba SC lilifungwa na Ramadhani Kipalamoto.
Matokeo ya jana dhidi ya Toto, yanaifanya Simba SC iporomoke hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake 35 baada ya kucheza mechi 21, nyuma ya Kagera Sugar yenye pointi 37, Azam pointi 43 na Yanga 49 kileleni. 

No comments:

Post a Comment