Pages

Sunday, March 31, 2013

KOCHA MARTIN O'NEILL AFUKUZWA KAZI SUNDERLAND



Sunderland iliyo katika nafasi ya hatari ya kushuka daraja imemfukuza kazi meneja wake Martin O'Neill kufuatia matokeo mabaya ya michezo mbalimbali ya ligi kuu ya nchini England.

Paka mweusi ana alama moja tu juu ya msatari wa kushuka daraja relegation zone ya Premier League relegation ikiwa pia imesaliwa na michezo saba jana ilipokea kichapo kingine cha bao 1-0 kutoka kwa Manchester United.

Sunderland haijashinda katika michezo nane mfululizo ya ligi kuu na katika jumla ya michezo yote hiyo imeambulia alama tatu.

Taarifa ya klabu hiyo imesema kuwa maamuzi ya nani atarithi mikoba ya O'Neill's yatafanyika katika siku chache zijazo.

Paolo Di Canio mwenye umri wa miaka 44, anatajwa kuwa mrithi wake.

Meneja huyo wa zamani wa West Ham United aliondoka katika klabu ya League One ya Swindon mwezi Februari, ambayo ilikuwa ni klabu yake ya kwanza kama meneja.

Pia meneja wa zamani wa timu ya taifa ya England Steve McClaren, ambaye naye aliondoka kibaruani FC Twente mwezi February, anahusishwa na kuchukua nafasi hiyo ya kazi.

Majina mengine ni pamoja na meneja wa zamamni waklabu za Queens Park Rangers na Manchester City  Mark Hughes na Roberto Di Matteo ambaye alitwaa taji la mabingwa Ulaya na michuano ya FA akiwa kama meneja wa muda wa Chelsea msimu uliopita.

Mchezaji wa zamani wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer, ambaye kwasasa yuko katika klabu ya nchini Norway ya Molde, pia anahusishwa na kazi hiyo kama ilivyo kwa bosi wa Brighton, Gus Poyet.

No comments:

Post a Comment