Pages

Sunday, March 31, 2013

LIVERPOOL YAIBANJUA ASTON VILLA IKISAWAZISHA NA KUONGEZA BAO LINGINE


Aston Villa imeshindwa kujiondoa katika eneo la hatari la uwezekano wa kushuka daraja katika ligi ligi kuu ya chini England ‘Premier League ‘ kufuatia Liverpool ilitokea nyuma kimatokeo kuibuka na ushindia wa mabao 2-1 mchezo uliofanyika Villa Park.



Kikosi cha Paul Lambert kilianza kuandika bao la uongozi kufuatia mpira wa Gabriel Agbonlahor kumkuta Christian Benteke aliyeandika bao hilo.



Liverpool ilisawazisha muda mfupi baada ya mpira kuanza kati pale ambapo Jordan Henderson alipo uchopu mpira uliompita mlinda mlango Brad Guzan.



Naye Steven Gerrard aliandika bao la pili kwa njia ya penati kufuatia Nathan Baker kumuangusha Luis Suarez katika eneo la hatari.

No comments:

Post a Comment