Pages

Sunday, March 31, 2013

TAMASHA LA PASAKA LAFANA LICHA YA MVUA KUNYESHA SIPHO MAKABANE , ROSE MHANDO WAKOSHA NYOYO ZA MASHABIKI


Rose Mhando

Sipho Makabane

Sipho akitoa burudani huku akisindikizwa na waimbaji wengine wa Tanzania

Umati ulikuwepo Taifa

 Kwaya ya Ambassador ya Rwanda wakitumbuiza
Anastazia Mukabwa akiwa na wacheza shoo wake

Upendo Kilahiro akitoa burudani

Boniface Mwaitege akiwa amewabeba wacheza shoo wake




Kama kawaida Rose akishambulia jukwaa
LICHA ya mvua iliyonyesha kutwa leo jijini Dar es salaam haikuweza kuzuia umati wa watu wa Mungu kuhudhuria tamasha la paska lililofanyika kwenye Uwanja wa Taifa

Tamasha hilo ambalo limeandaliwa na kampuni ya Msama Promotions, Mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Kayanza Pinda ambaye alikuwa amefuatana na mkewe mama Tunu

Awali akizungumza na umati huo Waziri mkuu alimsifu Msama kwa moyo wake wa kujitolea kwa kusaidia watu ambao hawana uwezo japo alichonacho siyo kikubwa.
"Nampongeza sana Msama kwa moyo wake wa kusaidia wengine kwani anasomesha watoto 40 na sasa anafanya matamasha ili kusaidia watu wengine ambao hawana uwezo hivyo na mimi nampa milioni 10", alisema Pinda

Waimbaji waliopanda kutumbuiza waliweza kukonga nyoyo za mashabiki kiasi cha kushangilia bila kukoma. Miongoni waliokonga nyoyo ni Sipho Makabane toka Afrika ya Kusini, Rose Mhando,Ambassodar kwaya toka Rwanda na wengine wengi

No comments:

Post a Comment