Pages

Sunday, March 31, 2013

DAVID BECKHAM ANAFIKIRIA KUONGEZA MKATABA PSG


 David Beckham ameweka wazi amedhamiria kuongeza muda wake wa kusalia katika klabu ya Paris St-Germain ya nchini Ufaranza mpaka msimu ujao.

Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya England baada ya kumaliza makataba wake katika klabu ya Los Angeles Galax alikuwa na ofa za vilabu kumi na moja kwa mkataba wa miezi mitano lakini chaguo lake lilikuwa ni PSG.

Amenukuliwa na Le Parisien akiuliza

"Ni nani asiyependa kuwepo sehemu kama hii? Ni sehemu ambayo ambayo kila mtu anataka kuwepo.".

Kocha wa PSG cCarlo Ancelotti amesema kuwa "ningependa kuona David Beckham akiongeza mkataba"

Ndani ya kipindi alichokuwepo Paris, Beckham amechangia kuivusha PSG ikitinga robo fainali ya vilabu bingwa Ulaya na sasa ikisubiri mchezo dhidi ya Barcelona na wakati huo huo PSG ikisalia katika kilele cha msimamo wa ligi kuu nchini Ufaransa Ligue 1.

Beckham ametoa kauli hiyo Ijumaa baada ya mchezo dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi ya nchini humo Montpellier ambapo walichomoza na ushindi wa bao 1-0 ambapo aliingia dakika 18 za mwisho katika mchezo huo.

Anatarajiwa kuwa msaada mkubwa katika mchezo dhidi ya Barca akitoa mchango kama mchezaji mzoefu.

No comments:

Post a Comment