Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao alilofunga Haruna Niyonzima |
Mshambuliaji wa Yanga Hamis Kiiza na beki wa Azam, Hamis Mcha
Mshambuliaji wa Yanga Hamis Kiiza akiwa na mpira huku beki wa Azam, Hamis Mcha akimzuia wakati wa mchezo wa ligi kuu uliochezwa uwanja wa Taifa
Haruna Niyonzima akishangilia bao kwa staili ya aina yake
TIMU ya Yanga leo imeibuka na pointi tatu kwenye mchezo wao dhidi ya Azam FC uliochezwa uwanja wa Taifa.
Yanga ambao walionekana kushambulia sana mwanzoni lakini baada ya dakika 20 walionekana kusimama kana kwamba wanatazama mechi na Azam kuwashambulia lakini umakini wa washambuliaji uliwakosesha mabao ya wazi.
Baada ya kosakosa hizo dakika ya 32 mshambuliaji wa Yanga Hatuna Niyonzima aliwainua mashabiki wa Yanga kwenye viti baada ya kuunganisha pasi ya Jerryson Tegete na kuandika bao la kwanza na la pekee kwa mchezo huo.
No comments:
Post a Comment