Diamond
akiwa na demu wake mpya.. Uhusiano wao huu umeanza kwa mbwembwe nyingi, ingawa
jamaa anazuga kama kawaida yake.
MSANII
wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul, Diamond, ameshangaza watu kwa kitendo
chake cha kuendekeza kuvua nguo watoto wa watu, ikiwa ni tabia inayozidi kuota
mizizi kwa mkali huyo.
Diamond
na Jokate Mwigelo enzi za uhusiano wao
Hadi
sasa, Diamond ametoka kimapenzi na wasichana kibao, akiwamo Wema Sepetu, Jokate
Mwigelo na sasa yupo na Vj Penny, uhusiano ulioanza kwa mbwembwe
lukuki.
Wema
Sepetu, akiongea kwa jazba.
Jana
usiku alipokuwa akizungumza katika kipindi cha mapenzi kinachorushwa na Clouds
FM, kinachoongozwa na mtangazaji wake, Diva, Diamond alionekana kujikanyaga
zaidi kwa kushindwa kuzuia hisia zake kwa akina dada.
Diva
alimuuliza Diamond idadi aliyowavua nguo mabinti, swali ambalo lilionyesha
kuwakera watu wengi waliokuwa wakifuatilia. Kwa kipindi cha miaka miwili sasa,
stori zote za msanii huyo zimekuwa zikihusiana na wanawake kama ilivyokuwa
kwenye nyimbo zake nyingi kuwa za mapeni.
Hata
hivyo, anapobanwa, mkali huyo hudanganya kuwa ni rafiki tu ingawa baada ya muda
mchache hutoa ukweli wote. Wakati anaanza kuwa na Wema Sepetu, Diamond
alikanusha kila wakati, hata hivyo baadaye alikuwa wazi.
Na
alipoachana naye na kuanza uhusiano na binti Mwigelo, alikuwa akifanya siri hadi
pale alipokuwa wazi, ingawa uhusiano wake haukudumu sana. Kwa kiasi kikubwa,
Diamond amekuwa akiibua maswali mengi kutoka kwa wadau wake wakitaka kujua kuwa
kama ataendelea kuwavua nguo akina dada hadi wakati gani?
Uhusiano
wake mpya na VJ Penny, utachukua muda gani kwa msanii huyo anayetamba na nyimbo
mbalimbali, vile Mbagala, Kesho, Kamwambie, Nataka Kulewa na nyinginezo
zinazofanya vyema katika vituo vya redio na televisheni.
No comments:
Post a Comment