Ligi kuu ya Tanzania jana ilichezwa kwenye viwanja tofauti na kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini
Mbeya mabingwa watetezi wa taji Simba walikuwa wageni wa maafande wa jeshi
la magereza Tanzania Prisons mchezo ambao ulimalizika kwa Simba kuibuka na
ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na kiungo Amri Kiemba.
Matokeo ya mchezo huo yanaifanya Simba ifikishe
jumla ya alama 31 hivyo kuibua matumaini ya kuendelea kulitetea taji lake,
kufuatia kupata sare mfululizo kabla ya mchezo wa leo.
Katika uwanja wa Azam Complex kule Mbande nje kidogo
ya jiji la Dar es Salaam wenyeji Azam fc ambao ni wawakilishi wa Tanzania katika
michuano ya kombe la shirikisho walikuwa wenyeji wa JKT Ruvu ambapo wamefanikiwa
kuichapa kwa mabao 4-0.
Mabao ya Azam yamefungwa na Hamisi Mcha, John Bocco
na Abdi Kassim.
Azam kwa mara nyingine ineendelea kuikaba koo Yanga
katika usukani wa msimamo wa ligi wakiwa wote wana alama sawa
36.
Matokeo ya kushangaza ni katika uwanja wa CCM
Kirumba Mwanza ambapo wenyeji Toto Afrikas walikuwa wakicheza dhidi ya Afrika
lyon ya jijini Dar es Salaam ambapo Lyon imefanikiwa kupata ushindi wake wa tatu
tangu kuanza kwa ligi kuu msimu huu baada ya kuifunga Toto nyumbani kwa mabao
2-0.
Katika uwanja wa Mkwakwani
jijini Tanga wenyeji Coast Union ya huko ilikuwa dimbani dhidi ya JKT Oljoro ya
Arusha ambapo dakika 90 za mchezo zimeshuhudia Coast wakiibuka na ushindi wa
mabao 2-0 mabao hayo yakifungwa Selemani Kassim Selembe na Jerry
Santo.
Kwa matokeo hayo ni kwamba Coastal sasa imefikisha
jumla ya alama 30 ikiwaa nyuma alama moja kwa Simba.
No comments:
Post a Comment