ALVES AMTAKA NEYMAR BARCELONA
Mlinzi
wa kimataifa wa Brazil na Barcelona Dani Alves amemtaka mshambuliaji wa Santos
na timu ya taifa ya Brazil kujiunga naye katika timu yake ya Barcelona wakati huu ambapo kuna
tetesi kuwa kigogo hicho cha Hispania kinatengeneza mazingira mazuri ya kujenga
hatma njema ya baadaye ya kinda huyo.
Neymar
amekuwa mchezaji bora kwa miaka miwili mfululizo wa bara la Amerika Kusini.
Alves
alishindwa kuficha juu ya hisia zake katika jaribio lake la kuendelea
kumshawishi Neymar mwenye umri wa miaka 20 kujiunga Nou
Camp.
Lakini
wakati tetesi nyingine juu ya mshambuliaji huyo kutaka kuelekea Ulaya baada ya
michuano ya kombe la dunia mwakani na kujiunga na Manchester City au Bayern
Munich kama ilivyokuwa inaarifiwa , Alves anasema atahakikisha mipango hiyo
inashindwa.
No comments:
Post a Comment