Shrikisho la soka duniani FIFA limepitisha matumizi ya kutumia teknolojia ya kuthibitisha mpira kuvuka mstari na kuingia golini ( Goal-line Teknoloji 'GLT') katika fainali ya kombe la dunia nchini Brazil 2014.
Taarifa iliyochapishwa katika mtandao wa shirikisho hilo imesema
"Baada ya jitihada za kuhakikisha teknolojia hiyo inajaribiwa na kuona kama inafaa kupitia michuano ya kombe la dunia la vilabu nchini Japan Desemba mwaka jana 2012, FIFA imeamua kuanza kutumia GLT katika michuano ya kombe la shirikisho nchini Brazil june 2013 and baadaye fainali ya FIFA ya kombe la dunia 2014 nchini Brazil.
Imekaririwa taarifa hiyo ikisema
"Lengo ni kutumia GLT ili kusaidia waamuzi na kupanda mfumo katika viwanja vyote”
FIFA pia imezindua zabuni ya imealika watu wote wenye kutengeneza na kutoa huduma ya mfumo huo wa goal-line technology kuomba kupewa kandarasi hizo huku maamuzi ya aliyeshinda yakitarajiwa kutolewa mwezi April.
Mifumo ya Hawk-Eye na GoalRef yote tayari imepitishwa na FIFA, ambayo inatumia kamera ikihusisha nguvu ndogo za mafasa ya kunasa nguvu za sumaku kuzunguka goli ambapo ndani ya mipira kutakuwa na saketi inayowashwa kwa lengo la kunasa mawasiliano(siyo tafsiri rasmi).
No comments:
Post a Comment