Pages

Friday, January 11, 2013

YANGA YAMALIZA KAMBI KWA KUFUNGWA 2-0 NA EMMEN FC YA DARAJA LA KWANZA

Young Africans imepoteza mchezo wake wa mwisho wa  kirafiki dhidi ya timu ya timu ya Emmen FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uholanzi, baada ya kufungwa kwa mabo 2-0 katika mchezo uliofanyika katika mji wa Bereke kwenye viwanja vya Arcuda foootball Antalya. 
Young Africans ilianza vizuri kipindi cha kwanza na kutengeneza nafasi za kufunga lakini kutokuwa makini kwa washambuliaji wake Nizar Khalfani, George Banda na Saimon Msuva kuliinyima Yanga kupata bao katika dakika 15 za kwanza, 
Dakika ya 23 Saimon Msuva alishindwa kuipatia Yanga bao baada ya kushindwa kumalizia pasi safi nzuri ya Nizar Khalfani ambapo Msuva aliupiga mpira na kuokukolewa na mlinda mlango wa timu ya Emmen FC.
George Banda ambaye leo alianza kama mshambuliaji wa kati akisaidiana na Nizar Khalfani alishindwa pia kuipatia Yanga bao baada ya kushindwa kumalizia mpira uliopigwa na Haruna Niyonzima akitokea upande wa kushoto wa uwanja
 Mlinda mlango wa Yanga Said Mohamed alifanya kazi ya ziada kuokoa mipira miwili ya hatari langoni mwake baada ya washambuliaji wa Emmen kugongeana vizuri na kuwatoka walinzi wa Yanga lakini mashuti yao walikuta yakiishia mikononi mwake. 
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans 0 - 0 Emmen FC.
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko ya kikosi chote ambapo waliingia, Yusuph Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Ladslaus Mbogo, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Godfrey Taita, Omgea Seme, Didier Kavumbagu, Jerson Tegete na David Luhende.
Yanga ilianza tena mchezo kwa utulivu huku ikipanga mbinu za kuweza kupata bao la mapema lakini umakini wa walinzi wa Emmen Fc ulikuwa kikwazo kwa washambuliaji wa Yanga kuweza kuipita ngome hiyo.
Emmen FC waliitawala zaidi sehemu ya kiungo hali iliyopelekea kufanya mashambulizi mengi langoni mwa timu ya Yanga, na katika dakika ya 73 waliweza kujipatia bao la kwanza baada ya mfungaji kumalizia krosi iliyowapita walinzi wa Yanga.

Dakika nne (4) baadae, Emmen FC walijiapati bao la pili ikiwa ni dakika ya 77 baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo wa Emmen FC kumponyoka mlinda mlango Yusuph Abdul na kugonga mwamba wa juu kabla ya mshambuliaji wa Emmen FC haujaukwmishwa wavuni na kuhesabu bao la pili.
Jerson Tegete aliumia dakika ya 79 katika harakati za kfunga na nafasi yake kuchukuliwa na Rehani Kibingu laikini mabadiliko hayo hayakuisadia Yanga kubadilisha matokeo.
Mpaka dakika 90 zinamalizika Young Africans 0 - 2 Emmen FC.
Mara baada ya mchezo kocha mkuu Ernest Brandts alisema amesikitishwa na matokeo hayo, timu yangu ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na kuwabana vizuri wapinzani wetu lakini kipindi cha pili umakini ulikosekana hali iliyopelekea kufungwa mabao mawili ya haraka haraka.
Makosa yaliyojitokeza katika kipindi cha pili tumeyaona kwa pamoja na benchi zima la ufundi hivyo tutayafanyia kazi yasijitokeze tena katika michezo itakayofuata alisema 'Brandts' .
 Yanga kesho itafanya mazoezi ya mwisho asubuhi kabla ya kuanza kujiandaa na safari ya nchini Tanzania siku ya jumapili mchana ambapo itarajiwa kufika Dar es salaam majira ya saa 10 kasoro ikiwa ni siku ya jumatatu alfajiri.
Kikosi kilichoanza kipindi cha kwanza: Said Mohamed, Juma Abdul, Stephano Mwasika,  Nadir Haroub 'Cannavaro', Shadrack Nsajigwa, Nurdin Bakari, Saimon Msuva, Frank Domayo, Geroge Banda, Nizar Khalfani,  Haruna Niyonzima
Kikosi cha kipindi cha pili: Yusuph Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Ladislaus Mbogo, Kelvin Yondani, Athuman Idd 'Chuji, Godfrey Taita, Omega Seme, Didier Kavumbagu, Jerson Tegete/Rehani Kibingu, David Luhende

No comments:

Post a Comment