Young Africans ilianza vizuri kipindi cha kwanza na
kutengeneza nafasi za kufunga lakini kutokuwa makini kwa washambuliaji
wake Nizar Khalfani, George Banda na Saimon Msuva kuliinyima Yanga
kupata bao katika dakika 15 za kwanza,
Dakika ya
23 Saimon Msuva alishindwa kuipatia Yanga bao baada ya kushindwa
kumalizia pasi safi nzuri ya Nizar Khalfani ambapo Msuva aliupiga mpira
na kuokukolewa na mlinda mlango wa timu ya Emmen FC.
George
Banda ambaye leo alianza kama mshambuliaji wa kati akisaidiana na Nizar
Khalfani alishindwa pia kuipatia Yanga bao baada ya kushindwa kumalizia
mpira uliopigwa na Haruna Niyonzima akitokea upande wa kushoto wa
uwanja
Mlinda mlango wa Yanga Said Mohamed
alifanya kazi ya ziada kuokoa mipira miwili ya hatari langoni mwake
baada ya washambuliaji wa Emmen kugongeana vizuri na kuwatoka walinzi wa
Yanga lakini mashuti yao walikuta yakiishia mikononi mwake.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans 0 - 0 Emmen FC.
Kipindi
cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko ya kikosi chote ambapo
waliingia, Yusuph Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Ladslaus Mbogo,
Kelvin Yondani, Athuman Idd, Godfrey Taita, Omgea Seme, Didier
Kavumbagu, Jerson Tegete na David Luhende.
Kikosi cha kipindi cha pili:
Yusuph Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Ladislaus Mbogo, Kelvin
Yondani, Athuman Idd 'Chuji, Godfrey Taita, Omega Seme,
Didier Kavumbagu, Jerson Tegete/Rehani Kibingu, David Luhende
Yanga
ilianza tena mchezo kwa utulivu huku ikipanga mbinu za kuweza kupata bao
la mapema lakini umakini wa walinzi wa Emmen Fc ulikuwa kikwazo kwa
washambuliaji wa Yanga kuweza kuipita ngome hiyo.
Emmen
FC waliitawala zaidi sehemu ya kiungo hali iliyopelekea kufanya
mashambulizi mengi langoni mwa timu ya Yanga, na katika dakika ya 73
waliweza kujipatia bao la kwanza baada ya mfungaji kumalizia krosi
iliyowapita walinzi wa Yanga.
Dakika nne (4)
baadae, Emmen FC walijiapati bao la pili ikiwa ni dakika ya 77 baada ya
mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo wa Emmen FC kumponyoka mlinda mlango
Yusuph Abdul na kugonga mwamba wa juu kabla ya mshambuliaji wa Emmen FC
haujaukwmishwa wavuni na kuhesabu bao la pili.
Jerson
Tegete aliumia dakika ya 79 katika harakati za kfunga na nafasi yake
kuchukuliwa na Rehani Kibingu laikini mabadiliko hayo hayakuisadia Yanga
kubadilisha matokeo.
Mpaka dakika 90 zinamalizika Young Africans 0 - 2 Emmen FC.
Mara
baada ya mchezo kocha mkuu Ernest Brandts alisema amesikitishwa na
matokeo hayo, timu yangu ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na kuwabana
vizuri wapinzani wetu lakini kipindi cha pili umakini ulikosekana hali
iliyopelekea kufungwa mabao mawili ya haraka haraka.
Makosa
yaliyojitokeza katika kipindi cha pili tumeyaona kwa pamoja na benchi
zima la ufundi hivyo tutayafanyia kazi yasijitokeze tena katika michezo
itakayofuata alisema 'Brandts' .
Yanga kesho
itafanya mazoezi ya mwisho asubuhi kabla ya kuanza kujiandaa na safari
ya nchini Tanzania siku ya jumapili mchana ambapo itarajiwa kufika Dar
es salaam majira ya saa 10 kasoro ikiwa ni siku ya jumatatu alfajiri.
Kikosi kilichoanza kipindi cha kwanza:
Said Mohamed, Juma Abdul, Stephano Mwasika, Nadir Haroub 'Cannavaro',
Shadrack Nsajigwa, Nurdin Bakari, Saimon Msuva, Frank Domayo, Geroge
Banda, Nizar Khalfani, Haruna Niyonzima
No comments:
Post a Comment