BEI YA FOMU ZA KUOMBA KUGOMBEA TFF YATAJWA, UCHAGUZI KUFANYIKA FEBRUARI 24 MWAKA HUU
|
Deogratius Lyato. |
SHIRIKISHO la soka nchini TFF limetangaza uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo ni Februari 24, mwaka huu ambapo utafanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa kamati ya uchaguzi ya TFF Degratius Lyato amesema fomu za kuwania
nafasi ya urais, makamu wa Rais na ujumbe wa kamati ya utendaji zitaanza
kutolewa Januari 14 ambapo zoezi hilo litaendelea mpaka Januari 18
katika ofisi ya katibu mkuu wa shirikisho hilo na idara ya uhasibu
kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 10 jioni.
Amesema
kwa nafasi ya mwenyekiti fomu hizo zitauzwa kwa shilingi laki 5, makamu
wa Rais shilingi milioni 2 wakati ambapo kwa nafasi ya ujumbe fomu hizo
zitauzwa kwa shilingi laki 2.
Mbali
na hilo pia kutakuwa na uchaguzi wa viongozi wa bodi ya inayosimamia
ligi uchaguzi ambao utafanyika februari 22 ambapo fomu kwa upande huo
zitaanza kutolewa januari 14 mpaka 18.
Amesema nafasi zinazogombewa ni mwenyekiti wa bodi na makamu mwenyekiti ambapo ada ni shilingi laki 2.
Amesema kwa wale wanaotaka nafasi ya kamati ya uongozi ada itakuwa ni shilingi laki moja.
Pia
Lyato amesema kwa mujibu marekebisho ya katiba ni kwamba mwenyekiti na
makamu wa mwenyekiti bodi hiyo watakuwa moja kwa moja ni wajumbe wa
kamati ya utendaji ya TFF na kwamba chaguzi zote zitafanyika jijini Dar
es Salaam.
No comments:
Post a Comment