Pages

Tuesday, January 15, 2013

MICHAEL WAMBURA ATUPA KARATA YAKE TFF, SAFARI HII NI KWENYE NAFASI YA MAKAMU WA RAIS

Michael Wambura akizungumza na waandishi baada ya kutoka ndani ya ofisi za TFF kuchukua fomu
Wambura akipanda gari lake mara baada ya kuchukua fomu kwenye ofisi za TFF
Michael Wambura akiongea na waandishi wa habari.
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Michael Richard Wambura na baadaye alikutana na vizingiti lukuki kila alipokuwa anajitokeza kuwania uongozi wa mpira katika ngazi mbalimbali, hii leo amejitokeza tena kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya makamu wa Rais wa shirikisho hilo.
Akionekana ni mwenye matumaini makubwa mara hii na maamuzi yake hayo, Wambura amesema kwasasa amekamilisha jukumu la kwanza la kuchukua fomu kama raia mwenye haki ya kufanya hivyo na kwamba mikakati ya kuelekea katika mchakato mzima wa uchaguzi kwa upande wake ndio unaanzia hapo. 
Amesema angependelea zaidi watanzania wangejitokeza kuchukua fomu ili kuleta changamoto kubwa zaidi katika mchakato mzima wa uchaguzi huo.
Amempongeza Rais wa sasa Leodgar Tenga kwa kuamua kuachia nafasi hiyo na kwamba hiyo inaonyesha ni namna gani Tenga alivyo muumini mzuri wa vipindi japo katiba haikumzuia na kuruhusu mawazo mapya na mfumo mpya na watu wapya ili kumpokea nafasi yake.
Amesema unapokuwa madarakani yapo ambayo utayafanikisha na mengine mazuri watu wayaenzi na yale aliyoshindwa wengine watayapokea kuanzia hapo na kuyaendeleza.
Pia sababu ambazo zimemfanya kuchukua fomu siyo za wakati ule na kwamba kila jambo lina wakati wake na pengine sababu ambazo zilikuwa zikionekana ni tatizo kwa wakati ule huenda zisiwe hivyo kwasasa.

Wambura amedokeza sababu zilizomsukuma kuwania nafasi hiyo ya makamu wa Rais kwakuwa ni nafasi ambayo ina changamoto nyingi na kwamba kuna mengi ambayo hayajafanyiwa kazi kwa kuwa nafasi hiyo haijapata mtu muafaka na wale wanaomaliza muda wao wanahitaji kusaidiwa.
Ameizungumzia pia sifa ya Rais ajaye kuwa anatakiwa kuwa amechaguliwa kwa mujibu wa katiba na kuupenda mpira wa miguu.
Awe ni mwenye kuelewa kuwa mpira wa miguu unatakiwa kuchezwa nchi nzima kwa kuwa ni mchezo unaopendwa na wengi kote nchini, vilevile awe na muda wa kuushughulikia mchezo wa soka na mwenye kiu ya maendeleo ya soka.
Amesema kuna haja ya kubadilisha mfumo wa soka uliopo ili kuwa na mpira ulio bora, timu ya taifa bora na kutoa nafasi kwa walio wengi kuucheza mpira wa miguu.

Wambura aliwahi kugombea nafasi ya Mwenyekiti Mkoa wa Mara lakini alienguliwa kutokana na kamati ya uchaguzi kusema kuwa hakuwa muadilifu kabla ya kutaka kujaribu tena bahati yake katika Chama cha soka Mkoa wa Dar es Salaam DRFA ambapo baadaye aliamua kujitoa na kuelekea katika kamati ya rufaa inayoongozwa na Profesa Mgongo Fimbo ambayo ilimsafisha.
 
Hata hivyo TFF ilipinga maamuzi hayo na kuelekea Shirikisho la Soka duniani FIFA kuomba mwongozo ambapo FIFA iliagiza TFF kuunda kamati ya rufaa inayojitegemea, kwasasa mabadiliko hayo yamefanyika.

Wambura yuko safi baada ya maamuzi ya kamati ya rufaa ya Prof Mgongo Fimbo.

No comments:

Post a Comment