Pages

Friday, January 25, 2013

AFRICAN LYON: HAKUNA KUSHUKA DARAJA TUTAPAMBANA HADI MWISHO YAONGEZA 12 KUKIPA NGUVU KIKOSI


Obadia Mungusa watatu kutoka kushoto akijifua kwa nguvu zote ili kurejesha heshima yake iliyopotelea Msimbazi.

Juma Seif Kijiko watatu kutoka kushoto naye akijifua kuhakikisha analinda heshima yake na klabu yake ya Lyon.

Semmy Kesi na Idrisa Rashidi nyuma yao ni Obina wakimsikiliza kaimu kocha wao Charles Otieno.
Wakati mzunguko wa pili wa ligi kuu ya soka Tanzania bara unaanza kesho kwa vilabu mbalimbali kushuka dimbani, Afrikan Lyon ambayo iko katika nafasi ya p;ili kutoka katika mkia wa ligi hiyo imejidhatiti vilivyo kuhakikisha inadondosha mmoja baada ya mmoja ili kujiweka katika nusura ya kushuka daraja daraja.

African Lyon ndiyo klabu iliyoongoza kwa kusajili wachezaji wengi kwenye dirisha dogo kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom utakaotoa bingwa wa Tanzania Bara, lakini pia timu tatu ambazo msimu ujao zitarudi kucheza Ligi Daraja la Kwanza.

Kati ya wachezaji 65 waliotua katika klabu mbalimbali katika dirisha hilo, Lyon ndiyo iliyoongoza kwa kuwanasa 12. Miongoni mwao hao, wawili (Ibrahim Job na Shamte Ally) imewachukua kwa mkopo kutoka Yanga.

Pia watano imewapandisha kutoka katika kikosi chake cha U 20. Wachezaji hao ni Nurdin Musa, Salvatory Jackson, Mohamed Athuman, Athuman Kajembe na jarufu Kizombi. Wengine walioingia katika timu hiyo katika dirisha dogo ni Juma Seif (Huru), Buya Jamwaka (Burkina Faso), Takang Valentine (Huru) na Yusuf Mgwao (Huru).

Akiongea hii leo mara baada ya mazoezi ya asubuhi jembe jipya la klabu hiyo Juma seif Kijiko amesema haoni sababu kwanini timu hiyo ishuke daraja wakati usajili wa dirisha dogo umefanyika vizuri.

Amesema uwepo wa wachezaji kama Mungusa, Idrisa Rashid, Yusufu Mgwao, Shamte na Ibrahim Job kama timu itashuka basi itakuwa ni aibu kwao na si timu ndio maana wamepania kuhakikisha kazi inafanyika na wapenzi wa soka wataiona.

Kwa upande wake Mungusa amesema anaamini kikosi ni kizuri isipokuwa kilichobaki ni kazi ya uwanjani na wote kwa ujumla wana hasira na timu hiyo ambayo imeingia katika damu yao ndani ya kipindi kifupi sana.

Kwa upande wake kaimu kocha wa klabu hiyo ambaye pia ni mkurugenzi wa ufundi Charles Otieno amesema nguvu kubwa imetumika kujenga kikosi imara na kwamba anaamini kama mpira utakuwa ni wa haki basi watakuwa katika hali salama ya kutokushuka daraja na pengine kutoa changamoto kubwa kwa vilabu mbalimbali.

Afrikan Lyon Kesho inaanza duru la pili la ligi kuu dhidi ya Simba katika mchezo utakaochezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Nayo Polisi Morogoro katika kuhakikisha inaondoka mkiani mwa ligi imesajili wachezaji wanane katika dirisha dogo kama ilivyofanya Oljoro JKT ya Arusha.

Wachezaji wa kigeni walioingia katika dirisha dogo ni Humphrey Mieno, Brian Umony, Jockins Atudo (Azam), Donald Obimma na Ulugbe Chika (Toto Africans), Zuberi Hamis na Tinashe Machemedze (Coastal Union), Musa Mudde na Abel Dhaila (Simba).

No comments:

Post a Comment