Pages

Friday, January 25, 2013

TAMASHA LA WASANII WA FILAMU KUFANYIKA DAR LIVE KESHO

Rais Shirikisho la Filamu Tanzania (TFF), Simon Mwakifamba akiongea mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani).
Msanii Vitalis Maembe akionyesha mfano atakavyokamua siku hiyo.
Dude akitoa kionjo cha nyimbo yake atakayoitambulisha kwa mara ya kwanza siku hiyo.
Baadhi ya wasanii hao wakisikiliza mawaidha kutoka kwa rais wao.
Waandishi wa habari wakichukua matukio ya ishu hiyo.
RAIS wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TFF), Simon Mwakifamba, amezungumzia juu ya maandalizi ya tamasha la wasanii wa filamu Bongo, walivyojiandaa kwa makamuzi ya nguvu Jumamosi hii ndani ya Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mbele ya wanahabari, katika viwanja vya Leaders Club leo, Mwakifwamba alisema maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika na kila kilichopangwa kitafanyika. Katika upande wa burudani, kutakuwa na wasanii mbalimbali waliojitolea kusapoti tamasha hilo ambao ni Vitalis Maembe, Mrisho Mpoto, Scorpion Girls, Dude, Mtunisi, Radon, Ray, JB, Wema, Jack Wolper, Uwoya, Dk Cheni, na wengine kibao.

No comments:

Post a Comment