Pages
▼
Wednesday, December 12, 2012
WACHEZAJI STARS WAWASILI KAMBINI KWA MAFUNGU
Wachezaji waliowasili kambini mpaka sasa ni walinda mlango Juma Kaseja, Mwadin Alli na Aishi Manua.
Walinzi waliofika ni Shomari Kapombe, Samir Nuhu, Erasto Nyoni, Issa Rashidi, Aggrey Moris na Amir Maftaha. Nadir Haroub 'Kanavaro' na Kelvin Yondani na Nassoro Masudi Cholo bado hawajafika ila Cholo ni mgonjwa.
Viungo waliowasili ni Frank Domayo, Salum 'Abubakar sureboy', Athumani Iddi 'Chuji', Amri Kiemba na Hamisi Mcha Hamisi. Shabani Nditi, Mrisho Ngasa na Mbwana Samatta bado hawajafika
Washambuliaji ni John Bocco, Simon Msuva na Mwinyi Kazimoto. Thomas Ulimwengu naye bado hajafika.
Baada ya mchezo dhidi ya Zambia tarehe 22/ 12/ 2012, timu hiyo itarejea tena kambini Januari 6 mpaka 20 ikiwa na wachejaji 18 kwa ajili ya michezo ya kujipima nguvu na timu tatu ambazo kocha Kim Poulsen ametaka atafutiwe timu zitakazo shiriki michuano ya wachezaji wa ndani ( CHAN )
Stars inakabiliwa na michezo kadhaa ya kuwania kucheza kombe la dunia ambapo mwezi March itakuwa na kibaru cha awali dhidi ya Morocco kabla ya mchezo wa marudiano utakaochezwa mwezi June.
Mwezi huo huo itakuwa na mchezo mwingine dhidi ya Ivory Coast kuwania kucheza kombe la dunia lakini pia kutakuwa na mchezo mwingine dhidi ya Uganda wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika UGANDA
No comments:
Post a Comment