Pages

Wednesday, December 12, 2012

UCHAGUZI TWFA KUFANYIKA MOROGORO DESEMBA 19

Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu kwa Wanawake Tanzania (TWFA) unatarajia kufanyika Desemba 19 mwaka huu mjini Morogoro.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Ombeni Zavala, uchaguzi huo utatanguliwa na Mkutano Mkuu wa TWFA. Wajumbe wapiga kura wote wa mikoa iliyofanya uchaguzi wake na kutoa taarifa za uchaguzi wao ofisi za TWFA wanatakiwa kufika Morogoro siku moja kabla (Desemba 18 mwaka huu).

Wagombea waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ni kama ifuatavyo; wanaowania uenyekiti ni Isabela Kapera, Joan Minja na Lina Kessy. Rose Kissiwa ni mgombea pekee wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti.

Wanaowania ukatibu mkuu ni Amina Karuma na Cecilia Mkafu. Nafasi ya mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inagombewa na Zena Chande pekee baada ya Furaha Francis kujitoa kutokana na sababu za kifamilia.

Sophia Charles na Triphonia Temba wanawania nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya chama hicho.

Wagombea Rahim Maguza, Macky Mhango na Rose Msamila wameondolewa kwa kushindwa kikidhi matakwa ya Katiba ya TWFA Ibara ya 28(2).

No comments:

Post a Comment