Pages

Wednesday, December 12, 2012

SIMBA YAANZA VEMA KUTETEA KOMBE LA MASHINDANO YA UHAI, COASTAL UNION NAYO USIPIME



TIMU ya Simba B leo imeanza vema kutetea kombe la  mashindano ya uhai kwa kuifunga African Lyon mabao 2-1 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Karume asubuhi.

Mashindano haya yamedhaminiwa na kampuni ya Bharessa kupitia bidhaa yake ya maji ya uhai alianza juzi na yanachezwa kwenye viwanja vya Karume na Chamazi.

Mchezo huo wa kundi B ulikuwa wa ushindani na kila timu ilikuwa ikifanya mashambulizi kwa zamu.

Simba ndio ilikuwa ya kwanza baada ya kufunga bao la kwanza dakika ya 15 kupitia kwa Miraji Athuman na la pili lilifungwa na Ramadhan Mzee dakika ya 42.

Bao la African Lyon lilifungwa na Ndela Kashakala dakika ya 50.

Baada ya mchezo kumalizika makocha wa timu zote walilalamikia maamuzi ya waamuzi kuwa yalikuwa na walakini pia kocha wa Simba alisema kuwa anashukuru kwani timu yake ilikuwa haijafanya mazoezi.




Mchezo wa jioni Coastal Union waliifunga Azam FC bao  1-0, bao lililofungwa dakika ya 80 na Benja Ngasa baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Azam

Kwenye michezo wa juzi, Mtibwa ambao walicheza jioni kwenye uwanja wa Karume waliifunga JKT Ruvu bao 3-1.

Mabao ya Mtibwa yalifungwa na Hillary Kapera dakika ya 22, Godfrey Mohamed dakika ya 50 na Richard Jacob dakika ya 89 kwa njia ya penalti.

Bao pekee la JKT Ruvu ambao ndio walikuwa wa kwanza kufunga lilitiwa kimiani na Richard Msenye dakika ya 20.

Timu ya Coastal Union ilishida bao 2-1 dhidi ya Tanzania Prison kwenye mchezo uliochezwa juzi asubuhi kwenye uwanja wa Karume.

Mabao ya Coastal Union yalifungwa na Ramadhan Shame dakika ya 24 na Yusuf Chuma dakika ya 33.

No comments:

Post a Comment