Pages

Wednesday, December 12, 2012

SIMBA YAPATA KOCHA MPYA

BAADA ya klabu ya Simba kuachana na kocha wake Milovan Circkovic ambaye ameikacha klabu hiyo bila sababu za kueleweka, taarifa za ndani za awali zinasema klabu hiyo imeamua kumuajiri kocha wa zamani wa Paris Saint-Germain na Asec Memosas ya Ivory coast ambaye ni raia wa Ufaransa.

Patrick Liewig aliyezaliwa mwaka 04/10/1950 kwasasa akiwa na umri wa miaka 62 ndiye kocha mtarajiwa wa wekundu hao wa Msimbazi na anatarajiwa kuwasili nchini wakati wowote kuanzia sasa kuanza kibarua hicho.

Uchunguzi umebaini kuwa kocha huyo atakuwa ndiye kocha mwenye mshahara mkubwa kuliko makocha wote wa kigeni walioko nchini kwasasa wakifundisha vilabu mbalimbali vya ligi kuu.

Kocha huyo kwasasa atakuwa anatokea katika klabu ya El Gawafel Sportives de Gafsa(EGS) inayoshiriki ligi kuu ya Tunisia ambako ilimwajiri tarehe 20.10.2012 na kudumu nayo kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Kabla ya hapo alitokea katika klabu ya MC Algier ya Algeria ambako aliajiriwa kama meneja 01/07/ 2012 ambako pia alidumu kwa mwezi mmoja kabla ya kuelekea EGS Gafsa).

Ni kocha mzoefu katika soka la Afrika licha ya kufundisha zaidi timu za Tunisia ambapo alifundisha pia Club Africain ya Tunis kuanzia 19/04/2012 mpaka 30/06/2012 akiwa kama kocha wa muda pia amewahi kuifundisha Stade Tunisien ya Tunisia kuanzia 01/07/2009 mpaka 22/07/2011 kama meneja.

Kocha huyu amekuwa katika kipindi cha mafanikio zaidi katika kazi yake ya ufundishaji soka katika klabu ya ASEC Mimosas ya Ivory coast ambako alidumu kwa miaka zaidi ya saba baada ya kuajiriwa 01/09/2003 mpaka 2009 kabla ya kuelekea Stade Tunisien.

Kabla ya kuja barani Afrika alikuwepo Uarabuni kuanzia 01/07/2001 mpaka 29/08/2003.

Historia yake alianzia kuifundisha Paris Saint-Germain kama kocha msaidizi kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia 01.07.1999 mpaka 30.06.2002, kabla ya hapo akiwa katika kipindi cha kujifunza zaidi akiwa kama meneja wa daraja la chini 01/07/1989 mpaka 30/06/1999.
Pia amewahi kuzifundisha USM Malakoff  ya Paris na Al Wahda Club ya Abu Dhabi.

Uchunguzi umebaini kuwa kocha Patrick Liewig ambaye ni muumini wa mfumo wa 4-2-3-1  ni kocha mwenye wastani wa ushindi wa asilimia
30.77%  sare asilimia 38.46%  na kupoteza kwa asilimia
30.77%.

Katika kipindi chake cha kuifundisha Asec Memosas amefainikiwa kuingiza timu hiyo katika michuano ya vilabu bingwa Afrika mara saba na kufikia hatua ya nusu fainali moja mwaka 2006.

Katika miaka ya 2003, 2005, 2007 timu hiyo iliishia katika hatua ya makundi 2008 na miaka ya 2004 na 2009 aliisaidia kufikia hatua ya mzunguko wa pili.

No comments:

Post a Comment