Pages

Monday, December 10, 2012

MAULID MWIKALO ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA FRAT TABORA MJINI

Maulid Mwikalo

Maulid Mwikalo amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha waamuzi wilaya ya Tabora mjini kwenye uchaguzi uliofanyika jana, mkoani Tabora.

Uchaguzi huo ulifanyika shule ya msingi Gongoni na ulihudhuriwa na wajumbe 16.

Nafasi ya Mwenyekiti ilikuwa na wagombea wawili, ambapo Maulid Mwikalo alimbwaga Fredinandy Machunde kwa kura 10 dhidi ya 5 na kura moja iliharibika.

Makamu mwenyekiti ilichukuliwa na mgombea pekee Bella Husein aliyepata kura 11 za ndio na kura tano za hapana.

Nafasi ya Katibu Mkuu ilikwenda kwa Athuman Hussein ambaye alipata kura 10 huku mpinzani wake Shaban Masanda akiambulia kura sita.

Katibu msaidizi ni Maliyatabu Chobanga aliyepata kura 14 za ndiyo na mbili za hapana na mweka hazina ni Fredy Mwenisongole ambaye alipata kura 11 na mpinzani wake Nestory Rivangara alipata tano

Mwakilishi wa wanawake ni Justina Charles aliyepata kura 12 za ndiyo na nne za hapana na mjumbe wa Mkutano mkuu haikupata mtu mgombea Masud Ngeleja alipata kura saba za ndiyo na kura tisa zilimkataa

Akizungumza  kwa njia ya simu Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa uchaguzi, Mwahamed Seif alisema kuwa uchaguzi ulikuwa huru na kila mtu aliridhika na matokeo kwani hakuna malalamiko au rufaa iliyowasilishwa

No comments:

Post a Comment